Somo la 7/19
Ukurasa wa 3/5 Mada A: Umri 0-3Mada A: Umri 0-3
Lengo la kazi yako sio “kumfanya mtoto afurahi wakati wote”. Kama unaweza kupunguza pole pole athari kubwa ya mwitikio wa mtoto katika kutenganishwa, umemsaidia mtoto kuwa wa kawaida. Kujitenga kabisa hakusaidii, lakini kuwa na aibu kidogo na hisia kali ni kawaida – tofauti pekee ni namna hisia zilivyo na athari kubwa. Kuwa katika hali ya hofu kubwa unapoondoka chumbani sio kawaida, lakini kulia au masikitiko unapoondoka ni kawaida kabisa.
Hapa tuna mapendekezo unayoweza kuyatumia. Kitu gani kinasaidia inategemea sana uhusiano binafsi kati ya wazazi walezi na walezi na mtoto mchanga husika. Hivyo, usijaribu kufanya “jambo sahihi”. Jaribu kuwa na hisia, unganisha utatuzi katika njia yako mwenyewe, na andika kila siku kuhusu mtoto anaitikiaje katika jitihada zako.
- Tumia vipimo vitano vya “mwenendo salama wa mlezi” (tazama somo la 6, Utangulizi wa Mada B: Vipimo vya mwenendo salama wa mlezi). Ni vigumu kuwa karibu na mtoto anayejitenga au kukung’ang’ania mara kwa mara bila ya kuathirika vibaya. Unapaswa kuongea na wengine (mume, marafiki) mara kwa mara kuhusu namna unavyojisikia, ili uwe na furaha hata kama mtoto haonyeshi mwitikio wa kawaida.
- Tumia mgusano wa mwili – mgusano wa mwili kama kumsinga mtoto kumbeba mtoto kunaamsha ufanyaji kazi wa kawaida wa mfumo wa uhusiano wa karibu. Kuwa na subira, inaweza kuchukua miezi mingi au miaka kabla ya mtoto kuonyesha hali ya kawaida ya uhusiano wa karibu kama vile kufurahia kukumbatiwa, kumbusu, kukaa mapajani kwako, au kukumbatiwa kwa upendo (tazama somo la 5 kwa mfano).
- Kuwa mwangalifu sana na kuonyesha hisia, jazba na hata uitikiaji kupita kiasi unapowasiliana na mtoto. Unaweza kumuona mama tena katika sehemu ya kwanza ya Zoezi la Kumtazama Mtoto Kimya na kugundua namna anavyotumia sauti yake na lugha ya ishara kumuhusisha mtoto katika kuwasiliana naye.
- Muonyeshe mtoto kwamba “upo wakati wote” na tarajia awe na mahitaji makubwa kwa ajili ya ulinzi na kuwepo kwako kwa muda mrefu kuliko walionao watoto kwa kawaida.
- Cheza “mchezo wa kujificha” mara kwa mara na mtoto. Aina hii ya mchezo itamsaidia mtoto kustahimili kutenganishwa kwa kuwa na furaha na starehe. Pia, zoezi hili linamsaidia mtoto kuunda “uwakilishi wa ndani” wa kwako ambao upo wakati wote, na kufanya asitegemee sana kuwepo kwako. Pia unaweza kuficha vitu na kumuacha avitafute – hili pia linamsaidia mtoto kuelewa kwamba watu na vitu vipo pale hata kama huwaoni na kuwasikia.
- Kama mtoto ni mkubwa kiasi cha kuelewa: Badala ya kuondoka chumbani kwa mtoto wakati wakulala, unaweza kucheza mchezo huu: mtoto anapaswa “kukwambia uondoke” yeye mwenyewe chumbani, na kukuita urudi kama ataogopa. Kwa namna hii anaweza kuhisi kudhibiti kutenganishwa badala ya kutoonyesha “kutelekezwa”. Kisha unaweza kumsifia kwa kuwa shupavu kiasi cha kukuambia “uondoke chumbani” kwa kipindi cha muda mrefu. Unaweza kufunga kamba kwenye nguo yako ili mtoto aweze kukuvuta kurudi kitandani. Mchezo huu unafurahisha.
Unapokuwa umeamua jinsi utakavyojaribu kuunganisha mbinu hizo mbili, ziandike na kisha andika mtoto ameitikia zipi vizuri zaidi. Tumia simu yako ya mkononi kuchukua video fupi za mazoezi yako na ziangalie ili kuelewa namna mtoto anavyoonyesha hisia. Hakikisha unaziweka karibu sana ili uweze kuona uso na mwonekano wa watoto.
Hapa kuna video ya mlezi ambaye anaonyesha moyo. Tafadhali angalia jinsi mlezi anavyotumia sauti yake na kumbembeleza mtoto mchanga na kumfanya mtoto mchanga ajisikie yupo salama. Pia ni muhimu sana kwamba mlezi anajaribu kuweka mahusiano na mtoto mchanga kwa macho. Hii itamsaidia mtoto mchanga kujisikia kuwa na mawasiliano ya pande zote.
Kwa ujumla watoto wanaowekwa kwenye familia mlezi kabla ya miaka mitatu huwa wanabadilika katika uhusiano wao wa karibu. Watoto walio wengi wataweza kuwekwa kwa wazazi walezi wote wawili au mmoja kama vile ni wazazi wa mtoto. Mara nyingi watoto wachanga huacha mfumo wa kuwa karibu waliojifunza kutoka kwa wazazi waliowazaa na kufuata ule wa mlezi wa awali. Pia hupenda zaidi kuwa kama wazazi walezi wao katika tabia na maendeleo ya kijamii kuliko watoto wanaochukuliwa na umri mkubwa. Hata hivyo, unapaswa kumpa mtoto mchanga muda mrefu kukabiliana na kupoteza wazazi waliomzaa kabla hajaanza kujenga uhusiano na wewe kama mzazi mlezi.