Somo la 8/19
Ukurasa wa 2/3 Utangulizi wa Mada: Kutafakari maendeleo yako kitaalamuUtangulizi wa Mada: Kutafakari maendeleo yako kitaalamu
Njia nzuri ya kufanya tathmini hii ni kujadili na kutafakari katika kikundi kuhusu maswali yaliyowasilishwa hapa chini.
(Unaweza kurejea katika mwanzo wa mafunzo ambapo ulijibu Mahojiano ya Kadi ya Maelezo)
Mwalimu anaweza kukuuliza maswali na kuandika majibu yako. Toa majibu kwa mtoto mmoja mmoja kwa zamu.
Tafadhali tafakarini pamoja maswali yafuatayo:
UKUAJI WA MTOTO
- Je, unafikiri mtoto anahisi yuko salama katika familia yako?
- Je, unamuona mtoto anagundua na kujifunza, au hana usalama na anatafuta ulinzi?
- Je, ukuaji wa mtoto unaendelea kama ulivyotarajia?
- Ni maendeleo gani umeyaona katika tabia ya mtoto?
- Kitu gani bado ni kigumu kwa mtoto katika uhusiano wa kijamii?
- Kama wapo: Ushirikiano wako na familia ya waliomzaa mtoto ukoje?
- Je, umeshapata njia ya kushirikiana na wazazi waliomzaa?
- Uzoefu wako muhimu sana na mtoto ni upi – ukiangalia namna unavyotenda, kitu gani kimefanikiwa zaidi na kipi kinaonekana kutofanya kazi?
UHUSIANO WAKO NA VIONGOZI NA WATAALAMU
- Ushirikiano wako na mfanyakazi wa huduma za jamii wa mtoto uliendeleaje?
- Uhusiano wako na msimamizi au meneja wa familia mlezi uliendeleaje?
- Uliridhishwa na nini zaidi?
- Ungewaomba wakusaidie nini, ukizingatia ushirikiano wako – unahitaji nini zaidi ili kumlea mtoto?
UHUSIANO WA FAMILIA YAKO
- Ni kwa namna gani kulea mtoto kumeathiri uhusiano wako wa ndoa?
- Je, uhusiano wenu umeimarika au umekuwa mgumu zaidi?
- (Kama wapo): Je, ulezi umeathiri vipi uhusiano wako na mtoto au watoto wako mwenyewe?
- Watoto wako (kama wapo) wamejifunza nini kutokana na hilo – wamewajibika zaidi na kuelewa, au wanauona ulezi wako kama mzigo?
- Je, rafiki zako, ndugu na majirani wameelewa zaidi na kukusaidia kuhusiana na ulezi?
- Je, wazazi halisi walikubali mtoto aishi na wewe?
- Je, mtoto alipata uelewa mzuri wa kuwa mtoto anayelelewa?
- Ni yapi kati ya mambo yafuatayo unafikiri yameboreka, na yapi bado yanahitaji uzingativu wako?
TABIA YAKO YA ULEZI YA KUJENGA UHUSIANO SALAMA WA KARIBU
- Umeshafanikiwa kutabirika na kueleweka katika namna unavyomjibu mtoto?
- Umeshawahi kuwa na hisia?
- Umeshawahi kupatikana kwa mtoto pale alipokuwa akihitaji faraja?
- Ulishawahi kupata hisia pamoja na mtoto na sio kama ilivyo kwa mtoto?
- Umeshawahi kutafakari pamoja na mtoto kuhusu kile anachokihisi na kudhania, na anavyowaona wengine?
- Umejifunza nini kuhusu kufanya tabia ya ulezi salama?
- Ipi kati ya tabia hizi umeiona kuwa na changamoto zaidi kwa mtoto unayemlea?
KAZI YAKO NA UHUSIANO WA MTOTO NA WANAKUNDIRIKA
- Unaelezeaje uhusiano wa mtoto na wanakundirika wenzie?
- Je, mtoto ana marafiki na unamsaidiaje kwa hili?
- Nini ambacho bado ni kigumu kwa mtoto kupata marafiki na kuhusiana nao?
- Umeshafanya uhusiano mzuri na walezi wengine (walimu, kituo cha kulelea watoto,wafundishaji wa kazi nyingine za muda wa ziada?)
- Unadhani umefanikiwa kwa jambo lipi na lipi bado linahitaji uzingativu wako?