Somo la 1/19
Ukurasa wa 1/5: Utangulizi wa kujifunza kwako na maendeleo ya somoUtangulizi wa kujifunza kwako na maendeleo ya somo
Jinsi ya kutumia andiko hili:
Programu hii ya mafunzo imeandaliwa na kujaribiwa katika mazoezi ya kila siku na watu kama wewe: Wazazi walezi kutoka nchi kumi tofauti wanaofanya kazi na watoto wadogo waliowekwa mbali na nyumbani.
Watafiti wengi na wataalamu katika ukuaji wa mtoto wameeleza maarifa yao kuhusu yapi ni mahitaji ya watoto katika matunzo. Kupitia uonyeshaji katika video ya malezi bora, mapendekezo na majadiliano ya kikundi, utajifunza ujuzi mwingi kama mlezi. Watoto watajitahidi vizuri na kujifunza zaidi.
Mwishoni mwa kila somo, unaamua namna utakavyofanya mazoezi ya ulichojifunza wakati wa somo. Kujifunza kote huku kuna manufaa tu kama kunatumiwa katika kazi yako ya kila siku na kama unapanga namna ya kubadili mazoezi yako kama mzazi mlezi wakati unapitia programu.
Mada ya somo:
Katika somo hili la kwanza la mafunzo utaelezwa kwa mawazo ya msingi na maudhui ya programu hii ya mafunzo na namna unavyoweza kutumia programu. Pia utaelezwa mahojiano ya watu wawiliwawili na mzazi mlezi mwingine – ili kuelewa namna elimu uliyonayo katika maisha yako ilivyo muhimu – elimu ambayo ina manufaa katika kazi yako ya utaalamu kama mzazi mlezi. Utaelewa kinachotarajiwa kutoka kwako wakati unajifunza nadharia ya utaalamu wa malezi ya mtoto katika programu, na namna wewe na mwalimu wako mnavyoweza kusaidiana wakati mkitumia programu.
Malengo ya somo:
- Kuelewa namna ya kutumia programu ya mafunzo, jinsi ya kufanya kazi pamoja wakati wa kukutana katika masomo, na namna ya kufanya kazi katikati ya masomo ukiwa nyumbani.
- Kuelewa namna uzoefu wa maisha yako binafsi unavyotoa elimu ya utaalamu yenye thamani kwa kazi ya malezi