Somo la 3/19
Ukurasa wa 1/6: Kumpokea mtoto wa kuleaKumpokea mtoto wa kulea
• Kujenga utambuzi kuhusu namna watoto wanavyokuwa na hisia ya mabadiliko ya walezi.
• Kumsaidia mtoto kujisikia salama katika familia yako mlezi.
Katika somo hili la mafunzo utatambulishwa namna watoto wanavyoweza kujisikia kwa familia mpya na mazingira, na namna unavyoweza kumsaidia mtoto kujisikia salama katika mazingira mapya, familia yako mlezi.
Malengo ya somo:
Malengo ya somo ni kukupa uelewa wa namna watoto wanavyoitikia mazingira mapya, na kukupa mapendekezo ya kuendana na kipindi cha kwanza cha kupangiwa mahali pa kuishi.
Katika video hii ya mkufunzi wa SOS Fairstart, Husna kutoka Tanzania, anaelezea jinsi alivyofundisha kikundi chake cha walezi jinsi ya kumkaribisha mtoto mlezi kwa njia sahihi katika familia. Kumpokea mtoto ni njia ya utaratibu sio kwa mtoto peke yake bali kwa familia nzima. Husna anaelezea vizuri jinsi ya kujenga maelewano baina ya moja hadi mwingine.