Somo la 7/19

Ukurasa wa 4/5 Mada B: Miaka 3-18

Mada B: Miaka 3-18

HISIA ZA WATOTO KUTENGANISHWA KUANZIA UMRI WA MIAKA MITATU NA KUENDELEA
Watoto kuanzia miaka mitatu na kuendelea tayari wamewekwa kwa wengine tangu walipokuwa wadogo kama vile wazazi wao. Kama mtoto alikuwa katika uangalizi wako tangu akiwa mdogo, huenda akawa karibu na wewe katika namna ambayo watoto wa kawaida wanakuwa karibu na wazazi wao.

Watoto wakubwa zaidi ya miaka mitatu – wanapowekwa mahali pa kulelewa – wanakuwa na wazo la utambuzi zaidi kuhusu wao wenyewe na ugumu wa kutenganishwa wanaoweza kuupata. Wanakuwa tayari wana ukaribu kutoka kwa wazazi au wengine na kama wanatarajia kutojaliwa hili linaweza kusababisha matatizo zaidi ya kudumu. Kama mtoto amepata ugumu katika kutenganishwa-au kutenganishwa kwa muda mrefu – hatua ya huzuni na kupona inategemea utayari wa walezi kuzungumza kwa uwazi kuhusu mtoto anachokabiliana nacho.

TAFSIRI YA KIHISIA YA KUPOTEZA WALEZI WAZAZI: KUJIAMINI KIDOGO
Kwa kawaida watoto huathiriwa na matatizo au kutenganishwa kwa muda mrefu kwa kufanya ufafanuzi wa hisia: “Nimeachwa, hivyo lazima niwe nisiyependeka na nisiye na thamani”. Ni muhimu kuelewa kwamba tafsiri hiyo ni ya kihisia na haihusiani na utambuzi na maelezo ya mantiki waliyoyapata toka kwa walezi – ni hisia zaidi kuliko kitu mtoto “anachojua”. Mtoto anaweza kuwa amejifunza kurudia maelezo yote yenye mantiki yaliyotolewa na walezi, lakini hisia zinaweza kuwa bado zipo, na mtoto siku zote anaweza kuhisi aibu ya kuwepo na kukosa maana ya maisha.
MIKAKATI YA KITOTO YA KUEPUKA HISIA ZA KUTOTHAMINIWA
Hakuna mtoto anayeweza kuvumilia hisia hizi, hivyo watoto wanajenga ulinzi wa kisaikolojia ili wasijisikie hawana thamani na kutojaliwa. Ingawaje ulinzi huo unaweza kuonekana kutofanya kazi, hakika una mantiki: mtoto anajaribu kutafuta mkakati kujilinda mwenyewe asipate upotevu mwingine: Kwa kuwa watoto hawajakomaa, mikakati yao ya kuepuka maumivu inaweza kuwa ya kizamani. Lakini kumbuka kwamba ni suluhisho zuri analoweza kulipata mtoto wakati huo ili kuepuka huzuni na msongo. Unaweza kuona hisia hizo kwa watoto wote lakini katika watoto ambao walipata utenganishwaji mgumu wana hisia kali zaidi na wakati mwingine kuharibu na kutumia nguvu zote ambazo zingetumika kwa kucheza na kujifunza.

  • Baadhi ya watoto wanakataa kabisa kuzungumza kuhusu siku za nyuma ili wasiwe na hisia hizo.
  • Baadhi ya watoto wanafanya “ubeuzi usio sahihi”: chochote kinachotokea wanaonekana watulivu na kuwa na mtazamo wa chuki kwa wito wote wa kuwa karibu na wengine “hata hivyo sijali kuhusu wewe au marafiki au mtu yeyote yule. Sijali kitu chochote, naomba uniache!” (tazama mkakati wa kuepuka kuwa na uhusiano wa karibu katika somo la 9). Mtazamo huu unaeleweka kwa sababu unamlinda mtoto asipate upotezaji mpya na kuwaweka wengine mbali – kuwapoteza hakutakuwa na maana.
  • Baadhi ya watoto wanakuwa wanajitegemea zaidi na “wakati wote anakuwa msichana mzuri/mvulana mzuri”, wanatumia nguvu zao zote kukubaliana na wanaowalea. Wanajaribu kuepuka mgogoro wowote na kuacha kuwa na maoni ya huru kuhusu chochote au kutokubaliana na wanaowalea – Niambie nifanye nini, mimi mwenyewe sijui”. Kwa kawaida wanahofia kufanya maamuzi kwa sababu hili linaweza kupingana na matarajio ya wengine.
  • Baadhi ya watoto wanakuwa “wanajiamini kuwa wakamilifu”: wanajaribu kufanya chochote kuzidi kiasi na kuzingatia katika kuangalia kama wamefanya mambo kwa usahihi. Wanahofia hata kufanya makosa madogo au kutotenda kikamilifu. Changamoto yoyote ndogo au kosa wanalofanya huwafanya kukata tamaa “Chochote nitachofanya, siko sahihi, mimi ni mtu aliyeshindwa, siwezi kitu chochote hata nikijitahidi namna gani. Mimi ni mjinga, nataka kufa, n.k.
  • Baadhi ya watoto mara nyingi wanakuwa na wasiwasi na kuwa na msongo na kukosa utulivu. Hawawezi kukaa kutulia na kamwe hawapumziki, na huweza kuongea wakati wote katika namna ya kuonyesha kuwa wana shughuli nyingi, ikionyesha wazi kuwa hii ni zaidi ya mtoto mwenye bidii, ni mtoto ambaye hawezi kupumzika kwa muda na kujaribu kutokumbuka siku za nyuma.
  • Baadhi ya watoto wanakuwa “wapweke”: Wanajitenga wenyewe kwenye vyumba vyao peke yao na kompyuta zao au midoli na kukataa kutoka nje au kuwakaribisha watoto wa rika lao. Wanachukia matukio yoyote ya kijamii au mialiko na kutafuta sababu ya kusema hapana. Wazo la hisia walizonazo ni kwamba “Kama sitakuwa na marafiki au kujumuika, hakuna atakayenikataa tena”.
  • Baadhi ya watoto wanakua kwa kuwachukia au kuwakasirikia wazazi wao au wengine ambao wametenganishwa nao. Hii inaweka maumivu ya kuwakosa.
MJADALA WA WAZI UNAWASAIDIA WATOTO KUTATUA NA KUKABILIANA NA KUPOTEZA WAZAZI: KUTOA NAFASI YA MJADALA WA WAZI
Utafiti katika hisia za kutenganishwa unaonyesha wazi: umuhimu wa mjadala wa wazi kutoka kwa walezi: Wakati wowote mtoto anapozungumza au kufanya akiwa na uzoefu wa kutenganishwa, anatambua hisia na mawazo kuhusu anachokipata. Hisia za kupoteza wazazi zinapungua nguvu zaidi na zaidi kila wakati, na kumbukumbu na uelewa vinakaa vizuri. Hadi mtoto anapofikia kiwango sawa na watoto wengine na anaweza kuhisi huzuni ya kawaida ambayo haisumbui hali yake ya akili na hamu ya kucheza, kugundua na kujifunza. Madhumuni ya kazi yako sio kuondoa huzuni zote, bali kumsaidia mtoto kuwa na hisia zisizo kali sana na zenye vurugu.

Pia utafiti unaonyesha kwamba kama walezi wanakataa, kupuuzia au kujaribu kuona upotezaji wa wazazi wa awali kitu kidogo, watoto hawataimarika katika kukabili hisia zao na hili linaweza kuharibu maendeleo yao ya haiba. Kwa mfano: Watoto wanapoasiliwa au kuwa katika ulezi hapo nyuma, hiyo ilikuwa ni aibu kubwa na kinyume na desturi za jamii. Hii iliwafanya watoto wahisi kunyanyapaliwa na mara nyingi walipata mshituko wanapokuwa wakubwa kiasi cha kuelewa kwamba “hawakuruhusiwa kuwa walivyo”. Matokeo yalikuwa ni kwamba watoto wengi walipata kiwewe kikubwa na walikuwa na maisha duni sana. Moja ya malalamiko katika mahojiano na walioasili na watoto wa kulea ni ya kawaida: “Hakuna aliyezungumza nami kuhusu kitu kilichokuwa muhimu sana – ukweli wa kupoteza wazazi wangu”.

Hivyo kazi yako ya kitaalamu ni kujaribu kutoa nafasi pale mtoto anapojisikia huru na kukaribishwa kufanya mjadala kuhusu alichokiona siku zilizopita. Hili linaweza kutokea kupitia mazoezi mengi.

Unapaswa kuamua namna gani na lini utazungumza na mtoto kuhusu kupoteza wazazi. Mara nyingi ni wazo zuri unapofanya kazi za nyumbani – kwa mfano mtoto amekaa mezani anachora au kufanya zoezi la nyumbani, na unatayarisha chakula au hali nyingine ya kawaida ya kila siku kama vile kuzungumza kabla ya kulala. Haya yanaweza kuwa matukio mazuri kwa mijadala. Kuwa na subira – mchakato huu wa mjadala unaweza kuchukua wiki kadhaa au miaka. Kila wakati mtoto anapofikia hatua mpya ya upevukaji na ukuaji, anaweza kulizungumzia tena na kutafuta mitazamo mipya.

Angalia video hii ya Peter ambaye anaishi SOS Children’s Village ndani ya Arusha, Tanzania. Peter anaongelea juu ya kukulia kwenye mlezi mbadala na jinsi mlezi alivyokuwa makini na kumsaidia katika maendeleo yake na ustawi wake.

KUMFANYA MTOTO AZIONE HISIA ZAKE KAMA ZA KAWAIDA
  • Angalia orodha katika aya hapo juu: “Mikakati yakitoto ili kuepuka hisia za kutothaminiwa
  • Tafuta ni ulinzi upi dhidi ya hisia zilizotelekezwa unaona mara nyingi zaidi katika mtoto unayemuhudumia. Wakati wewe na mtoto mnapojisikia vizuri na una muda, mwambie mtoto kwamba unataka kuzungumza kuhusu namna mtoto anavyohisi wakati anapokosa mawasiliano na watu muhimu (mama, baba, ndugu wa baba mmoja au wanyama wa kufugwa waliokuwa karibu nao).
  • Elezea hisia unazofikiri mtoto wako anazo na mwambie kwamba hivyo ndivyo watoto wengi wanafanya wanapompoteza mtu muhimu. Kwa mfano: Wakati mwingine watoto wanampoteza mtu waliyempenda na wanahofia kumpoteza mwingine tena. Hivyo wanakataa kuongea na wengine na kukaa chumbani mwao siku nzima. Hivi ndivyo wanavyofanya watoto wengi na ninafikiri ni busara sana – kwa sababu kama wanakaa chumbani kwao peke yao na hawafanyi urafiki na yeyote, wanaweza kukataliwa tena. Ninaweza kulielewa hili vizuri sana!”
  • Au unaweza kumwambia mtoto “hadithi inayofanana” na ya utotoni mwako: Nilipokuwa na umri kama wako baba na mama yangu walikuwa na shughuli nyingi sana na mara nyingi niliachwa peke yangu. Nilipojaribu kutafuta urafiki na watoto wengine mara nyingi walikataa na kunifanyia fujo. Hivyo niliamua kukaa chumbani kwangu siku nzima – Sikutaka kuwasiliana na wengine kwa sababu nilikuwa na uhakika kwamba hawakunipenda au wangenikataa. Nilipokua niligundua kwamba watoto walio wengi wanafanya hivyo, na ninafikiri ni busara – kisha wanalindwa wasikataliwe tena”.
  • Unaweza kusoma au kutunga hadithi ya wakati wa kulala kwa ajili ya mtoto kuhusu mtoto aliyetelekezwa – Kama vila Oliver Twist (au mtu mwingine kutoka kwenye riwaya ya nchini mwako ambaye mtoto anaweza kujifananisha naye). Wakati unaendelea unaweza kumuuliza mtoto kama anatambua ni nini mtu huyo anahisi na kufikiri.
  • Unaweza kutumia midoli, michoro au udogo wa mfinyanzi kucheza na mtoto. Hadithi ambazo mtoto alitelekezwa au kupoteza wazazi na kupata njia ya kukabiliana na hali hiyo.
  • Pamoja na watoto wakubwa au vijana: Unaweza kumpa mtoto simu ya mkononi (au kamera yenye video) na kumsaidia kutengeneza filamu ndogo au mahojiano kuhusu namna alivyohisi kupoteza wazazi au wengine. Kama una intaneti, unaweza kumsaidia kijana kuwatafuta vijana wengine wanaolelewa na kuwasiliana nao kwenye Facebook au mitandao mingine.
  • Kama una mawasiliano mazuri na mwalimu wa shule ya mtoto: mwambie mwalimu atengeneze mada ya siku au mada ya wiki kuhusu “Kumpoteza mtu au kitu unachokipenda”. Kwa msaada wa mwalimu, watoto wote wanaweza kutoa mifano ya kupoteza mfano babu au mtu mwingine au kitu, kwa kutumia michoro, maigizo, n.k. Kisha unaweza kujadili na mwalimu jinsi ya kumsaidia mtoto kueleza kuhusu kumpoteza mtu.

 

Tafadhali andika namna, lini na wapi unaweza kutumia moja kati ya uchaguzi huu, au buni mmoja mpya, ambao matini hii inaweza kukuvutia. Andika baada ya kutumia mpango kazi wako: Ilikuwaje, mtoto alihisi vipi, kitu gani kilikuwa kigumu kwako, ulijifunza nini katika kujaribu, utaendeleaje?

TAMBUA NA KUSUBIRI MWITIKIO WA MTOTO
Sasa umetoa nafasi ambapo kupoteza mzazi kunaweza kuzungumziwa kwa uwazi. Hivyo usimwambie mtoto kwamba sio vizuri kukaa chumbani siku nzima, au kuanza kumpa ushauri, msikilize tu na muache mtoto azungumze kama anataka kufanya hivyo – huenda ikachukua siku moja au mbili kabla mtoto kufanya ulichokisema. Kama mtoto anaanza kuzungumza, itikia tu kwa kichwa na sikiliza kwa shauku na msifie mtoto kwa anachokifikiria au kuhisi.

Huenda hili ndilo unalotaka kufanya kwa muda mrefu mara ya kwanza: unamsaidia mtoto kupona kwa kuzungumza kuhusu kupoteza wazazi na kuonyesha kwamba uko tayari kushirikishana na kusikiliza.

TAJA FAIDA NA HASARA ZA MKAKATI WA MTOTO
Wakati una uhakika kwamba mtoto anahisi kwamba unamsikiliza kwa subira na kuelewa hisia zake, unaweza kuanza mjadala kuhusu faida na hasara za mkakati wa mtoto.

Kwa mfano:
Nilipokaa chumbani kwangu siku nzima nikichora, hakika nilikuwa mchoraji mzuri nilipokua. Hilo lilikuwa ni jambo zuri. Lakini pia nilikuwa mpweke sana kwa sababu sikuthubutu kutoka nje na kutafuta marafiki. Kila wakati nilipolifikiria hilo, niliacha kabla hata sijafungua mlango kwa sababu niliogopa kukataliwa au kudhihakiwa. Hivyo jambo baya lilikuwa kwamba sikuwa na wa kucheza naye, na shuleni sikuwaomba wengine kama tungeweza kuwa marafiki – unajua hisia hiyo?”

Kwa hilo unamuonyesha mtoto katika namna ya upole kwamba mkakati wake unaondoa hofu katika muda mfupi, lakini pia kumfanya mpweke kadri anavyoendelea. Kisha unaweza kuongea kuhusu namna watoto wanavyoweza kuogopa kukataliwa tena au kumpoteza mtu wanayempenda.

PENDEKEZA NJIA MBADALA ZA KUKABILIANA NA HOFU
Hatua inayofuata ni kumfanya mtoto afikiri njia nyingine ya kukabiliana na hofu ya kupoteza wazazi tena au kukataliwa tena.

Kwa mfano:
“Siku moja nilielewa kwamba ningekuwa mwenyewe maisha yote kama ningekaa mwenyewe chumbani kwangu. Nilikuwa na hofuia sana mtu kusema hapana kama nitamuomba kuwa rafiki. Lakini shangazi yangu aliniambia, kama unataka marafiki, huenda utakataliwa mara nane lakini ndiyo mara mbili, na hizo ndiyo mara mbili wanaweza kuwa marafiki zako wakubwa. Shangazi yangu aliniambia hakuna tatizo katika kulelewa na wengine, na kwamba hakuna sababu ya kuona aibu. Kwa hakika maelfu ya watoto wanaishi bila ya wazazi wao. Hivyo, nilianza kuwaalika wenzangu darasani kucheza nao baada ya masomo, na shangazi yangu alinisaidia kuzungumza nao. Wengi wao walisema hapana, lakini mmoja wao alisema ndiyo, na tulikuwa marafiki wakubwa kwa miaka mingi. Huenda utakuwa imara vya kutosha kukabiliana na hofu yako na kuanza kuwaalika wengine siku moja”.

Au:
“Unapohisi upweke unakuwa na hasira sana, kisha unaanza kuhoji, na kisha unahisi huzuni zaidi na hufai. Huenda unaweza kujaribu kusema kwamba uko mpweke, wakati mwingine una hasira?”