Somo la 10/19

Ukurasa wa 7/7: Mpango kazi: Mambo ya kufanya kabla ya somo linalofuata

Mpango kazi: Mambo ya kufanya kabla ya somo linalofuata

Tafadhali chagua moja kati ya mada hizi na andaa mpango kazi wake. Chagua mada unayoona iatumika sana kwa kazi yako ya sasa.

  • Jitahidi kumfanya mtoto ajisikie kwamba ana msingi salama na nafasi binafsi, na kwamba yeye ni mmoja kati ya wanafamilia mlezi. Je, hili litafanyikaje?
  • Andaa mpango wa kukutana kila wiki katika familia mlezi, ambako kanuni za tabia zinajadiliwa na kukubaliana na watoto wote na vijana katika familia. Je, utafanyaje hili?
  • Wazazi walezi: zungumzeni kuhusu namna watu katika mtandao wenu wa kijamii wanavyoweza kupata njia nzuri za kumuelewa mtoto na kukabiliana na tabia yake. Je, utazungumza na nani na wakati gani?

Andika kile ambacho wewe kama mzazi mlezi, umejadiliana na kuhitimisha na kuamua nani atafanya lipi.

Asante kwa utayari wako na kila la heri katika kazi yako hadi somo linalofuata!