Somo la 10/19
Ukurasa wa 4/7: Mada B: Kumpa mtoto sehemu yake binafsiMada B: Kumpa mtoto sehemu yake binafsi
Kila mtoto anapaswa kuwa na sehemu yake binafsi: Mhusishe mtoto katika kupamba chumba au sehemu yake mwenyewe. Mtoto anaweza kuwa na kiti chake mwenyewe katika meza wakati wa chakula cha usiku. Pengine anaweza kuwa na boksi binafsi linalofungwa au kabati, ambalo linaweza kufunguliwa na mtoto au wazazi walezi. Mtoto pia anaweza kuwa na muda wa uhuru binafsi: haki ya kupumzika katika chumba au sehemu ya mtu. Kwa watoto wenye jazba au matatizo ya tabia, hata shughuli ndogo – kama saa chache shuleni – wanaweza kuchosha sana. Matatizo mengi yanaweza kuzuiwa kama mtoto anajua kwamba “sasa nina muda wa saa moja kujipumzisha, kucheza au kufanya kazi yangu ya nyumbani”. Kujumuisha mapumziko ya mara kwa mara kwa muda binafsi kunaweza kusaidia sana. Watoto wenye matatizo ya kujali muda hupenda kukaa muda mfupi sana au mrefu sana kwenye vyumba vyao. Kwa hiyo, kukubaliana kuhusu ratiba kwa mapumziko madogo kunaweza kuzuia uchovu na gadhabu za hasira.
Kwa watoto wadogo na watoto wanaojifunza kutembea: Nafasi binafsi pia inaweza kuwa kitu kama vile mdoli au labda fulana yenye thamani, n.k. Jadili makubaliano nyumbani: wanafamilia wengine wataonyeshaje kwamba wanaheshimu umiliki wa mtoto wa kifaa? Kuwa na mnyama wako wa kufugwa – kama kuwajibika kutunza ndama, mbuzi, kuku au mnyama mwingine – kunaweza kuendeleza uhusiano wa karibu. Watoto wengi wanaanza mchakato wa uhusiano kwa kuwa karibu na mnyama. Hili linakuwa halina tatizo kubwa kama kuwa na uhusiano wa karibu na mtu.
Kumsaidia mtoto mdogo/mtoto anayejifunza kutembea kujijengea uwezo wa kujitambua: Kucheza na vioo, kumuacha mtoto kujisikiliza sauti yake mwenyewe kutoka kwenye simu ya mkononi, kinasa sauti kunaweza kusaidia utambuzi wa “Hey, hii ni yangu”! Katika kujumuika kilasiku, mzazi mlezi anaweza kuzungumza kila anachokifanya mtoto (“sasa unajaribu kufunga vifungo vya shati lako – sio rahisi sana, lakini endelea kujaribu). Kuzungumza kuhusu hilo ni njia nzuri ya kumsaidia mtoto kutambua namna vitendo vinavyowaathiri wengine, na namna ya kusikiliza, kufikiria na kujibu. Hii inamsaidia mtoto kuelewa namna ya kuenenda katika kujumuika. Kujua namna tabia inavyowaathiri wengine ni kitu ambacho watoto wasio na matumaini wanapata matatizo kuelewa kwa sababu wanapata mwongozo kidogo katika maisha yao ya awali. Unapompa mtoto majibu: zungumzia tu kuhusu mazuri na ujumuikaji wenye mafanikio zaidi. Usitaje majibu yoyote yasiyofaa. Lenga katika matendo mazuri.
Shughuli za watoto na vijana: Katika muda uliopangwa kila siku (wakati wa kulala ni mzuri), kuwa na mazungumzo mafupi na mtoto kuhusu kilichotokea wakati wa mchana (au chochote kilichomfurahisha mtu). Jadili na kukubaliana na mtoto namna ya kuliandika hili katika daftari binafsi. Polepole, muache mtoto mwenyewe aandike muhtasari mfupi. Kama mtoto ana matatizo ya kusoma, muhtasari unaweza kurekodiwa kwenye simu ya mkononi ya mtoto au ya kwako mwenyewe. Hili ni zoezi zuri la kupata mambo yote yaliyotokea wakati wa mchana, na kumfundisha mtoto kufikiria kwa utulivu anachokifikiria na anachokihisi. Licha ya hilo, zoezi hili linaboresha kumbukumbu na uwezo wa kuona mbele.
Kuzungumzia kuhusu sifa zipi alizonazo mtoto na kitu ni gani kinamfanya awe wa kipekee na tofauti na watoto wengine ni muhimu. Na pia ana sifa ipi katika namna anavyojumuika na wengine (“wakati wote unakuwa makini unapoongea na mimi, na unaniangalia machoni – hilo linanifurahisha!”).
Mlezi anachukua filamu ya shughuli ya mtoto
Dakika 10
- Mapendekezo haya yamekuhamasishaje? Unaweza kufanya nini nyumbani?
- Je, una taratibu nzuri, utamaduni au mawazo kwa ajili ya kuendeleza hisia ya mtoto ya kuwa na nafasi binafsi na kujisikia yuko nyumbani?
- Utamsaidiaje mtoto kujitambua zaidi, na kuelewa namna atakavyojumuika na watu wengine katika familia?
- Unafikiri ni shughuli gani zitamsaidia mtoto wako kutambua zaidi tabia yake mwenyewe, na jinsi gani tabia hizo zinawaathiri wengine? Kwa mfano: andika katika shajara kila siku, rekodi video kwenye simu yako ya mkononi, kucheza na kioo. n.k.