Somo la 10/19

Ukurasa wa 5/7: Mada C: Kumsaidia mtoto kujifunza kuhusu desturi, wajibu na tabia katika familia mlezi

Mada C: Kumsaidia mtoto kujifunza kuhusu desturi, wajibu na tabia katika familia mlezi

Kila familia ina mazoea na kanuni zake kwa ajili ya mienendo – namna tunavyo zungumza pamoja, tunavyoheshimiana, na taratibu za kila siku katika familia nakadhalika. Mara nyingi hatuyazungumzii hayo kwa sababu kila mwanafamilia anajua “hivyo ndivyo tunavyoenenda katika familia”. Lakini kwa mtoto anayetoka katika familia nyingine, au katika taasisi, au pengine kutoka kwa wazazi ambao walishindwa kumtunza, hata kanuni hizi nyepesi za maadili zinaweza kuwa ngumu kujifunza. Kama mtoto anayelelewa ana matatizo ya tabia, itakuwa ni vigumu kwa watoto wanaozaliwa na familia mlezi kuelewa ni kwa nini wazazi wao wanamtendea tofauti mtoto anayelelewa. Wanaweza kuwa na wivu, au kuogopa kwamba uangalifu wa wazazi wao uko kwa mtoto mgeni tu. Huenda pia wanaweza kukasirishwa na tabia ya mtoto (“Anaingia tu na kuchukua nguo zangu bila ya kuomba!”).

Kwa hiyo, ni muhimu kutafuta uwiano mpya. Wazazi walezi wanaweza kuweka kanuni mpya za maadili, kuzieleza kwa wanafamilia wote, na kuonyesha namna ya kuzitumia katika mazingira ya kila siku. Kufanya hivyo mara kwa mara kutamsaidia mtoto anayelelewa kujihisi kwama mwanafamilia, na kuwafundisha namna ya kuenenda.

Mkutano wa familia wa mara kwa mara kila wiki ili kutoa kanuni za namna ya kufanya kazi pamoja. Anza katika njia rahisi kwa kuuliza kwa mfano: Tutaheshimianaje? Ni muhimu kwamba mtoto ashiriki na kukubali. Kwa mfano: “Hebu tujadili na kupata kanuni tatu za namna ya kusaidiana” au “tunapokula chakula cha usiku, tunaweza kuelezana kwa zamu kila mtu siku yake ilivyokuwa? Au “Ingekuwa vizuri, kama mngeshirikiana vitu vyenu na midoli” au “Nina kanuni: Sote tufanye zamu ya kupanga meza ya chakula”. Unaweza kuchagua mada yoyote ambayo unafikiri itasaidia kuondoa migongano.

Mfano:

Mama mlezi mmoja anagundua kwamba vijana wawili walikasirishwa sana wakati watoto wadogo wanawafuata, hawawapi nafasi ya kuwa na faragha. Baada ya kulijadili hili na familia nzima jioni moja, aliweka kanuni kuhusu muda ambao vijana wanapaswa kuwa peke yao. Wakati wote kutakuwa na kutokubaliana katika familia. Ni muhimu kwa watoto kujua kwamba kuna seti ya kanuni na ni wakati gani na wapi tutashauriana kanuni na kujadili matatizo. Taratibu majadiliano yatawapa watoto uelewa mzuri wa namna ya kushirikiana.

Kwa watoto wanaolelewa ambao wamepata matatizo, kujifunza namna ya kujumuika kunaweza kuchukua muda mrefu kuliko kawaida.

Hapa kuna mfano wa mahojiano na wazazi walezi ambao walimpokea mtotoaliyekosa matunzo alipokuwa na mwaka mmoja na nusu:

”Nilipompokea, nilikuwa sitoki kabisa, alikuwa hajui kuongea, na alikuwa bado analishwa kwa chupa. Watoto wetu walikuwa wanatarajia kuwa na mdogo wao wa kiume, lakini alikuwa hawezi kuwajibu. Walipojaribu kumshika au kumpapasa, alianza kupiga kelele au kujaribu kuwakwaruza. Iliwachukua muda mrefu kuelewa kwamba alikuwa na uchangamshaji kidogo, na kwamba sisi kama wazazi walezi ilibidi tukae naye kwanza kwa muda mrefu. Kwa sababu tulimchangamsha mara kwa mara, ukuaji wake ulifanyika haraka sana – lakini yeye kadri alivyokua mkubwa, ilionekana wazi kwamba hakujua kujumuika: alikuwa mwenye nguvu sana, mgomvina kutotulia wakati wote. Hakuweza kukaa katika mazungumzo au shughuli kwa zaidi ya dakika moja. Mara nyingi aliacha alichokuwa akikifanya, au kuwakatisha wengine walipokuwa katikati ya mazungumzo. Kwa sababu aliogopa na kuwa na msongo wa mawazo, wakati wote alijaribu kuwadhibiti wengine na kuwatawala. Watoto wetu wakiwa na miaka mitano na sita, wakubwa kuliko yeye waliona ajabu sana kwamba mtoto anayejifunza kutembea angefikiri kutawala meza ya chakula, na kwamba angepiga tu kelele kama hakuruhusiwa kufanya atakacho, Hivyo, familia nzima ilibidi ijitahidi kumuonyesha namna ya kubadilika, kuwasikiliza wengine na kujibu katika mazungumzo. Pia alihitaji mwongozo zaidi ili kujifunza namna ya kuelewa ni wapi anapopaswa kwenda na asipopaswa. Leo hii ana miaka tisa na anaweza kwenda shule – lakini akiwa na msisimko, bado anakuwa kama mtoto wa miaka mine. Sasa anawaamini wanafamilia wote, anampenda sana kijana wetu mkubwa, na amejifunza kuomba msaada katika mazingira magumu. Walimu wake ni wavumilivu sana lakini pia wana msimamo imara, hivyo sasa anajifunza haraka sana kuliko hapo awali. Sisi kama familia tumejifunza kudhibiti hali ya shughuli nyingi za siku na jinsi ya kuzuia migogoro. Kwa namna fulani hili limetuweka sisi, watotowetu wenyewe na mtoto wetu mwingine tunayemlea kuwa karibu, lakini miaka miwili ya kwanza ilikuwa migumu sana kwetu.”

Hii ni mahojiano na Galus, ambaye amepata mafunzo ya SOS parental training. Galus anaelezea juu ya kuwa mlezi wa vijana na anaweka mkazo katika njia mbali mbali katika majukumu yake kama baba.

MASWALI YA KUTAFAKARI NA MAZUNGUMZO

Dakika 10

  • Umeshawahi kuwatunza watoto wa kulelewa ambao wana changamoto zinazofanana?
  • Familia yako ililipokeaje hilo na kujitahidi kuwasaidia kujifunza stadi za kujumuika?
  • Je, una mapendekezo yoyote au uzoefu wa namna ya kukaa na watoto wenye changamoto kama hizo kwa sababu ya kukosa matunzo kabla ya kuwapokea?
  • Utapanga kufanya nini nyumbani ili wanafamilia wote waweze kushirikiana kumsaidia mtoto kujumuika na wengine?