Somo la 19/19

Ukurasa 3/5 Mada A: Kutathmini ujuzi wako kutokana na kazi na mafunzo yako

Mada A: Kutathmini ujuzi wako kutokana na kazi na mafunzo yako

Kwa kila swali:

  • Tumia fomu iliyo katika ukurasa wa mwisho wa majadiliano ya ujuzi ulioupata.
  • Tafadhali tumia dakika tano kutafakari na kujadili kila swali hapa chini.
  • Kisha tumia dakika tano nyingine kujadili ni ujuzi upi ulioupata kama ujuzi wa ujumla wa wazazi walezi.

Mmoja wa washiriki anaweza kuandika na kuangalia muda.

Your content goes here. Edit or remove this text inline or in the module Content settings. You can also style every aspect of this content in the module Design settings and even apply custom CSS to this text in the module Advanced settings.

MAENDELEO YA UJUZI WA VITENDO NA UHUSIANO YA MTOTO ANAYELELEWA

Mtoto anaweza kuwa ana matatizo madogo au makubwa anapowekwa kwako, unapaswa kulizingatia hilo unapojibu maswali haya. Pia uzingatie umri wa mtoto:

• Unafikiri nini kuhusu maendeleo ya ujuzi wa vitendo wa mtoto – ambao mtoto anaimarika katika kujifunza kwa mfano kuvaa nguo mwenyewe, kuwa na mpangilio thabiti wa siku, kufanya kazi zake za nyumbani, kuendesha baisikeli, n.k.? Kwa kifupi, amejifunza kufanya mambo kwa vitendo mwenyewe, ukilinganisha na watoto wengine wa umri kama wake?

Tafadhali eleza ujuzi mlioupata kama wazazi walezi kutokana na uzoefu wako wa kila siku na mafunzo ya Fairstart katika kusaidia kukua kwa ujuzi wa uhusiano wa mtoto: Kwamfano: “Nimejifunza kwamba ni muhimu kuhisi na mtoto na sio kama mtoto – watoto kutoka katika uhusiano uliovunjika wanaweza kuitikia katika namna isiyo na mpangilio katika matunzo, na hatusumbuliwi tena na hili” Uwezo wa mtoto anayelelewa wa kukabiliana na kutengenishwa na kujenga utambulisho wa wazi: Je, mtoto anatambua namna kupoteza wazazi na kutenganishwa kulivyomuathiri? Je, mtoto amejenga uelewa wa namna ya kukabiliana na kutenganishwa? Je, mtoto bado anaonyesha mwitikio mkali wa kimwili na kihisia kwa kutenganishwa (kama vile hofu), au inawezekana kuwa mtulivu anapotenganishwa nawe au watu wengine muhimu? Je, mtoto anaweza kueleza namna anavyoweza kukabiliana na utenganishwaji?

Tafadhali eleza ujuzi mlioupata kama wazazi walezi kutokana na uzoefu wenu wa kila siku na mafunzo ya Fairstart katika kuwasaidia watoto kukabiliana na wasiwasi wa kutenganishwa: Je, mtoto ana wazo lolote kuhusu yeye ni nani? Je, mtoto anajua ni tofauti gani walezi wamechangia kwa jinsi alivyo leo hii? Je, mtoto anaweza kulieleza hili?

Tafadhali eleza ujuzi mlioupata kama wazazi walezi kutokana na uzoefu wenu wa kila siku na mafunzo ya Fairstart katika kuwasaidia watoto kujenga utambulisho wa wazi licha ya kuwa na mazingira tofauti: Kujenga mtandao wa kijamii wa mtoto: Kwa kuangalia uhusiano wako na mtandao wako wa ndani (ndugu zako, majirani, walimu wa shule, n.k.), tafadhali taja mada tatu muhimu katika ushirikiano wako ambazo zimekuwa msaada kwa mtoto.

Tafadhali eleza ujuzi mlioupata kama wazazi walezi kutokana na uzoefu wenu wa kila siku na mafunzo ya Fairstart katika kujenga mtandao wa kijamii unaokubalika na wa wazi ambao ni msaada kwa mtoto: Kwa kuangalia uzoefu wako katika kushirikiana na viongozi kuhusu kupangiwa mahali pa kuishi, tafadhali taja mada tatu muhimu katika ushirikiano wako ambao umekuwa msaada kwa mtoto.

Tafadhali eleza ujuzi mlioupata kama wazazi walezi kutokana na uzoefu wenu wa kila siku na mafunzo ya Fairstart katika kushirikiana na mamlaka: Kwa kuangalia ushirikiano wako na wazazi waliomzaa, tafadhali taja mada tatu muhimu katika ushirikiano wako ambao umekuwa msaada kwa mtoto.

Tafadhali eleza ujuzi mlioupata kama wazazi walezi kutokana na uzoefu wenu wa kila siku na mafunzo ya Fairstart katika kushirikiana na wazazi waliomzaa mtoto unayemlea. Kwa mfano: “Nimejifunza kumuonyesha mtoto kwamba tunawaheshimu wazazi wake licha ya matatizo na kwamba hili linasaidia mtoto kujiheshimu mwenyewe” (Kama ni muhimu kwa  upangiwaji huu wa mahali pa kulelewa): Kwa kuangalia kazi yako na kipindi cha mpito cha mtoto kuanzia utotoni hadi ujana na katika kuondoka kwenye uangalizi wako, tafadhali taja mada tatu muhimu ambazo zimekuwa msaada kwa kijana.

Tafadhali eleza ujuzi mlioupata kama wazazi walezi kutokana na uzoefu wenu wa kila siku na mafunzo ya Fairstart katika kumsaidia mtoto kupitia umri wa ujana na kuondoka kwenye ulezi.