Somo la 15/19

Ukurasa wa 5/7 Kuwaandaa vijana kwa wakati kabla ya kuondoka

Kuwaandaa vijana kwa wakati kabla ya kuondoka.

Kama ulivyosikia katika mahojiano na Saleh, alishiriki katika semina za SOS  za maandalizi ya vijana watanaotoka kwenye malezi ya makao.katika mahojianao yetu na vijana hao walihitimisha kwa kutoa ushauri kwa wafanyikazi:

  • “Hakikisha kwamba watoto na vijana walio katika matunzo kuweza kukutana na vijana wengine ambao wameondoka katika matunzo (makao) au wale ambao hawako katika malezi mbadala.
  • Wawaandae vijana jinsi watakavyoweza kuwajibika wao wenyewe.
  • Vijana wafundishe ujuzi wa kazi za jamii ili kuweza kuishi vizuri.
  • Vijana wapewe mwelekeo wa wazi na mifano kutoka katika maisha halisi.
  • Vijana watambulisha kwa watu muhimu katika jamii watakayoishi.
  • Wakusanye vikundi kuzungumza juu ya mada tofauti na kutumia video za kuelimisha na ziara kutoka kwa wataalam (watu wenye uzoefu wakuweza kuzuia uhalifu, kuzuia ujauzito wa mapema, VVU, COVID19). ”

    TUNAWEZAJE KUANDAA VIJANA? BAADHI YA MAWAZO YA KUFANYA NA KUPANGA

    Hapa kuna baadhi ya maoni kutoka kwenye miradi ya vijana wanaotoka kwenye matunzo(makao) ili kuhamasisha kazi yako:

    • Katika semina na mikutano, wafanyikazi wa SOSCV wanaweza kugawa vijana katika makundi. Wafundishe juu ya changamoto na shida katika maisha baada ya malezi.uliza kila kikundi kusoma somo, kujadili pia kuwasilisha suluhisho pia mikakati ya kukabiliana na hadhira. Wafanyakazi wanaweza kusikiliza na kutoa maoni baada ya mawasilisho.vijana wazoefu waliotoka kwenye malezi wanaweza kualikwa na kutoa mrejesho pia.
    • Mafundi wa ndani ya nchi na wanawake wanaofanya kazi ndani ya jamii wanaweza kualikwa kuwasilisha kazi zao na ujuzi wao, pia familia ya malezi wanaweza kuunganishwa na wafanyabiashara na wamiliki wa biashara. Vijana wanaweza kufanya kazi mahali kwa muda, ili kuona kaa kazi hii inaweza kuwa kazi yao baadaye ili kukidhi gharama za maisha baada ya maisha ya makao.

     

    KUSHEREHEKEA MABADILIKO KWENYE MAISHA WA KUJITEGEMEA

    Katika utamaduni wa jadi wa Kiafrika, ibada za jadi na sikukuu husaidia mabadiliko kutoka kuwa mtoto, kuchukua jukumu na majukumu ya Kiutu mzima. Ibada hizi zinaweka wazi kwa kijana na jamii nzima kuwa mtu huyo sasa ni mtu mzima anayejitegemea.

    Kufanya hafla ya kijamii kuashiria mabadiliko ni njia muhimu sana ya kutambua mabadiliko ya kisaikolojia. Unaweza kufanya hafla ya kusherehekea siku ya mwisho katika matunzo katika makao. – Hafla hizo zitasaidia vijana kujivunia hali yao mpya kama watu wazima wanaojitegemea ndani ya jamii. Kuandaa hafla ya kuaga kunaweza kuongeza ujasiri na hali ya kujitegemea kwa kijana. Kabla, walezi wanapaswa kukusanya picha zote, video, na rekodi zingine za kibinafsi kwa kuwekwa kwenye kijitabu. Mlezi mkuu anaweza kuandaa hotuba fupi, na kuzungumza juu ya jinsi kijana huyo amechangia maisha katika familia au kikundi wakati wa malezi. Anaweza kuelezea ustadi wa kijamii, nguvu na talanta za kijana. Kijana anaweza kutoa hotuba juu ya kile alijifunza wakati anatunza akiwa makao, na mipango ya baadaye. Vijana wengine au watoto wanaweza kuelezea jinsi mtu huyo ni rafiki mzuri. Wanafamilia na uhusiano wa baadaye katika jamii wanaweza kualikwa, kujadili baada ya hafla jinsi wanavyoweza kumsaidia kijana hapo baadaye.

    MJADALA WA KIKUNDI

    Dakika 10

    • Tunawezaje kuandaa vijana kwa kuwajulisha juu ya hatari, na kuwaunganisha na watu katika jamii muda mrefu kabla ya kuondoka?

    • Je! Tunawezaje kusherehekea watunza huduma, kuwawezesha kujithamini na hadhi yao mpya kama watu wazima wenye thamani?

    Umesoma na kujadili jinsi ya kujiandaa kwa kuondoka utotoni, katika miaka ya ujana, na kwa wakati ambapo kijana huaga kwa msingi wake salama. Sasa, wacha tuangalie jinsi kurudi kwa jamii baada ya huduma inaweza kupangwa?