Somo la 15/19
Ukurasa wa 1/7 Kuwandaa watoto wanaotoka kwenye malezi(makao) ndani ya jamiiKuwandaa watoto wanaotoka kwenye malezi(makao) ndani ya jamii
Uwezo na umahiri unaotakiwa kutekelezwa:
- Kuelewa mabadiliko kutoka malezi kwenda kwenye maisha ya utu uzima na maisha ya kujitegemea.
- Kuelewa changamoto kuu tatu kwa vijana wanaotoka kwenye makao Afrika Mashariki
- Tunaweza kujifunza nini kwa kuwasikiliza vijana wazoefu waliokuwa kwenye makao
- Kufundisha ujuzi juu ya kujitegemea kutoka utoto wao.
- Kuwaandaa vijana kwa malezi ndani ya jamii.
- Ushauri na ujumuishaji wa jamii baada ya malezi
Mada ya kipindi: katika kipindi hiki utajuzwa juu ya changamoto kuu za vijana wa Africa mashariki wanaotoka kwenye makao. Utapata msukumo wa kujadili na kuandaa vijana wanaotoka kwenye makao kwa maisha baada ya malezi ya makao- jinsi ya kuwaandaa kutoka utoto hadi kuwangoza katika maisha ya kujitegemea ndani ya jamii.
Malengo ya kikao: kusaidia kupanga na kutoa msaada kwa vijana wanaotoka kwenye makao kwa kuwaandaa watoto na vijana kwa maisha baada ya malezi ya makao.unaweza kuangalia mda oja au Zaidi kati ya hizi.
1. Kufundisha ujuzi juu ya kujitegemea kutoka utoto wao.
2. Kuwaandaa vijana kwa malezi ndani ya jamii.
3. Ushauri na ujumuishaji wa jamii baada ya malezi ya makao.