Somo la 20/21

Ukurasa wa 4/7: Mada B: Kujitayarisha kwa mazungumzo ya wazi na watoto wako na vijana

Mada B: Kujitayarisha kwa mazungumzo ya wazi na watoto wako na vijana

Kabla ya kuanza Mada B

Tafadhali fanya muhtasari mfupi kutoka kwa Mpango Kazi A kuhusu mada ambayo washiriki wanahitaji kujadili. Je, washiriki wowote wanaona haja ya kuzungumza na mwanasaikolojia? Hebu tuhakikishe kwamba Walezi wote katika kikundi chetu wanahisi wamejitayarisha vyema kwa ajili ya kuondoka, na tayari kupanga jinsi ya kuwafahamisha watoto.

 

Kuzuia kujirudia sonona kwa watoto

Watoto wanaopata malezi ndani ya Kijiji tayari wametenganishwa na wazazi na wenzao kabla ya kuingia katika Kijiji cha SOS. Mtoto anapoarifiwa kwamba ni lazima aondoke kwenye sehemu salama na uhusiano salama kwa marafiki na wafanyakazi katika makao aliyozoea, hofu na fikra za zamani kutokana na kutengana mapema na walezi na marafiki yanaweza kuamka na kuunda wasiwasi mwingi wa kujitenga, mfadhaiko na hisia zingine mbaya. Jibu hili linaitwa msongo unaojirudia. Mapendekezo na mijadala ifuatayo itakusaidia kuzuia msongo tena kwa watoto na vijana na kuwapa uzoefu mzuri kuhusu kuondoka.

Girl talks about moving out of the SOS Village with her SOS Mother and her dreams for the future.

Je! Watoto na vijana wako wataonesha mwitikio gani?

Kulingana na umri wao na historia, watoto wataonesha mwitikio wa tofauti sana kwa taarifa hii. Watoto wachanga na watoto wadogo wanaishi wakati huu, na watatarajia kukaa kwao kwa sasa kudumu “milele”. Watahitaji uhakikisho na uzoefu wa kimwili wa mazingira yao mapya ili kuelewa.

Watoto wakubwa na vijana wanaweza kuwa tayari wanatamani kuondoka Kijijini na kuwa sehemu ya jumuiya, lakini bado wanaweza kuhisi kutokuwa na usalama na hofu kuhusu mpito.

Chukua dakika 10 kutafakari na kuona namna gani watoto au vijana ulionao watakavyojibu maswali.

Kila mlezi  atafakari kuhusu mtoto au kijana kutoka kwenye makao yake:

  • Je, mtoto huyo au kijana huyo bado ana hofu na wasiwasi mkubwa wa kujitenga kutokana na mazingira alioishi kabla ya kujiunga katika makao mapya? Au ana furaha zaidi na anaendelea kuwa nayo hata pale ambapo hapajatokea jambo ambalo halijatarajiwa?
  • Je, mtoto huyu kwa kawaida hubadilika kuendana na mazingira au utaratibu wa kila siku? Kwa mfano, ilikuwaje alipoanza shule, au alipokutana na watu wapya katika maeneo mapya?
  • Ni matarajio gani ambayo mototo anayo na yanaweza kutekelezwa kwenye jamii au makao anayoishi?
  • Kutokana na uelewa wako kuhusu mtoto huyu, ni njia gani ya kuzungumza naye ambayo inaweza kuwa bora kwako na kufanya vizuri?

Dakika 30 za majadiliano kwenye vikundi.

Mwanakikundi mmoja anawasilisha mawazo yake kuhusu jinsi atakavyoongea na mmoja wa watoto wake walio wadogo kabisa au wakubwa kiasi wakati kikundi kinamsikiliza. Kisha, washiriki ndani ya kundi pia wakawasilisha fikra na mawazo yao ya njia gani nzuri na rahisi ya kuongea na mtoto. Mwanakikundi mwingine anawasilisha mawazo yake namna ya kuongea na motto mwenye umri wa juu kidogo au kijana anayeanza kubalehi. Washiriki wanasikiliza na kasha wanatoa maoni yao. Kwa hivyo tafadhali jadili:

  • Tunawezaje kuzungumza na mtoto au kijana, kulingana na jinsi alivyo na mahitaji yake binafsi?

 

Mpango kazi mada B: Kuzungumza na watoto na vijana

 

Ushauri wa msichana wa miaka 11 kwa watoto wenzake wanaoondoka kwenye makao: Kutokana na uzoefu wangu, wanapaswa kufanya kila wawezalo kushirikiana na wazazi kambo wao wa SOS. Hawapaswi kuogopa kuondoka, wanapaswa kufikiria kuwa: “Nitapata marafiki wapya, na kufaulu mitihani yangu, nitajaribu tu kufanya kila kitu kwa usahihi, ndipo nitakuwa na furaha

Hapa kuna maoni na ushauri wa majadiliano na mazoezi na shughuli za kuwafanya watoto na vijana kuelewa maana halisi ya kuondoka kwenye makao. Wanaweza kushirikishwa kikamilifu katika mchakato na kusikilizwa maoni na mapendekezo yao juu ya kuhama. Mpango huu wa kazi una hatua mbili.

Vitu ambavyo vinaweza kusaidia wakati wa mazungumzo

Mazingira ya kawaida na salama, nyumbani kwa mlezi wa kambo panaweza pakawa ni sehum sahihi ya kuanzisha mazunguzo kwa watoto kuhusu mipango ya kuondoka baadae. Tafuta muda kama mchana au jioni watoto wakiwepo. Mnaweza mkawa mnaburudika kwa chochote kama chai wakati huo.

    Helpful tips for informing children 

    Hii ni baadhi ya miongozo ya namna ya kuzungumza na watoto kuhusu kuondoka kwenye makao.

    • Chagua mahali muda ambapo wewe na watoto wako mna utulivu. Waambie simulizi kuhusu jinsi wewe mwenyewe ulivyopata uhamisho au kuishi mazingira tofauti katika utoto wako, na kile ulichojifunza kutokana na hili.
    • Waeleze watoto uwezekano wa kuhama wakati fulani katika siku zijazo  kwa njia ya utulivu na yenye kuleta matumaini.
    • Ikiwa kuna watoto wowote wanaoonesha kutokukubali na kwa, hofu au huzuni, waruhusu wakuonyesha hisia zao na kuzungumza juu ya maoni yao. Usiwazuie jaribu kuwashawishi kuhusu faida zake. Wape muda wa kujibu maswali yao ya papo kwa hapo.
    •  Wahakikishie watoto kwamba bado utakuwa mlezi  wao, sasa na hata katika jamii.
    • Waambie watoto kwamba utazungumza nao tena mara nyingi kabla ya chochote hakijafanyika.

      Baada ya kikao kwenye makao wanakikundi wanaweza kushirikishana yaliyojiri na pia kufanya tathmini ya zoezi zima.

      •  Je, watoto waliitikia vipi habari  za kuondoka?
      •  Je kuna motto yeyete walionyesha dalili za kupata msongo upya? Tunahitaji mtaalamu wa kuwahudumia baadhi wenye msongo?
      • Ni watoto gani wanaohitaji mazungumzo ya kibinafsi zaidi na walezi wao kila siku?
      • Ni maswali gani kutoka kwao ambayo tunapaswa kupata majibu?
      • Tulijifunza nini kutokana na kuwafahamisha watoto kuhusu kuhama kwenye makao/nyumbani kwa walezi?

         

        Hatua ya 2: Kikao cha pamoja cha kupeana taarifa kwa watoto wote ndani ya makao

        Mara tu baada ya mlezi mmoja au zaidi kuwapa taarifa watoto wao katika makundi, kikao cha pamoja cha kuwapa taarifa watoto wote kwenye makao kinapangwa. Kwa nini hiki kikao ni cha muhimu?

        Hata kama kuna mlezi mmoja anayepanga kuondoka kwenye makao, taarifa zitaenea kwa kasi sana miongoni mwa wafanyakazi wake. Kuepuka wasi wasi na sitofahamu itakayotokea kwa watoto ni vema kuandaa kikao kati ya walezi na watoto wote walioko kwenye makao ili kuwataarifu kuhusu jambo hili. Watumishi wengine kama meneja mradi na walimu wanaweza kushiriki kwa ajili ya kutoa michango yao kimawazo.

        Ufuatao ni ushauri kidogo, unaweza kuongeza chochote vile inavyofaa:

          • Watoto kutoka kila nyumba kwenye makao wawekwe kundi moja na walezi wao.
          • Mkurugenzi wa makao au meneja wa mradi sababu za na muda wa kuondoka kwenye makao
          • Mlezi wa zamani anaotoa uzoefu wake kama mmowapo wa jumuiya ya SOS
          • Kijana mmoja au wawili walioishi kwenye makao wanaelezea uzoefu wao kabla na baada ya kuondoka kwenye makao na walezi wao wanaelezea uzoefu wao wa kuishi nao kwenye makao.  Wanaeleza ni kwa namna gani walipata marafiki, pia walivyoanza shule, ni kitu gani walijifunza na ushauri wao kwa watoto wengine.

          Kazi ya kikundi. Dakika 15

          Watoto katika kila kikundi kujadili na kuuliza maswali kwa walezi wao na wale vijana wawili. Walezi wa SOS kuwasilisha maswali kwa hadhira, na majibu ya wafanyikazi husika.