Somo la 20/21

Ukurasa wa 5/7: Mada C: Kukaa kama familia ndogo ya kikundi katika jamii/makao

Mada C: Kukaa  kama familia ndogo ya kikundi katika jamii/makao

Kutoka kwenye kazi yako na mada A na B, Walezi wote na watoto sasa wana habari njema.

Tafadhali tumia dakika kumi kufupisha uzoefu wako kutoka mpango kazi B:

Tulijifunza nini kama Walezi kutokana na jinsi tulivyowaelezea watoto kuondoka kwenye makao?

Tulijifunza nini katika kikao cha kupeana taarifa kwenye makao?

Kuwajumuisha walezi na watoto katika jamii mpya

Kuna namna mbili muhimu za kufanikishwa kuingia  katika jamii mpya:

Walezi na watoto lazima wajenge mahusiano mapya na mitandao ya kijamii – na majirani na watoto wao, na viongozi wa mitaa, wachuuzi wa mitaani, walimu wa shule na wanafunzi. Kupokelewa kama mwanajumuiya mpya inahijtaji mipango.

Jambo la pili ni kuwajumuisha watoto na vijana katika kazi na shughuli za kila siku, na kuwapa majukumu. Ni hapo tu ndipo watakua na uwezo wa kujitegemea, na kuweza kuishi kama watu wazima katika jamii. Kwa watoto ambao walikuwa wamezoea aina nyingine ya majukumu ya kila siku katika makao, maendeleo haya mapya yanaweza kuwa changamoto.

 

Embu sikiliza uzoefu wa Mama Tulipo!

Mama Tulipo alianza kama mlezi wa SOS na baadae akawa mlezi wa kambo. Hapa anaelezea uzoefu wake binafsi jinsi alivyoimarika na maendelea chanya ya watoto wake wa kambo.

Mpango kwenye kikundi chetu: Tunawezaje tunawezaje kufahamiana na jamii mpya?

Uhitaji wa taarifa za wazi unahitajika wa watu wote ndani ya jamii. Bila kufahamiana, wanaweza kuwa na mawazo mabaya na chuki kwa walezi na watoto kaika jamii wanaokua bila wazazi.  Hapa kuna mapendekezo ya shughuli, mara tu nyumba ya familia inapochanguliwa – tafadhali ongeza mawazo yako mwenyewe.

1.  Vikao vya vikundi na viongozi ngazi ya jamii, viongozi wa serikali za mitaa na wataalamu wa ustawi wa jamii

Viongozi wa kidini na wa serikali katika jamii ni watu muhimu kwa kuleta mafanikio na msaada wa baadaye kwa wanakaya wa kikundi kidogo kwenye makao. Majadiliano ya vikundi kwa mwaliko kutoka kwa Mkurugenzi au Meneja mradi/msimamizi wa mradi yanaweza kupangwa na kiongozi mmoja baada ya mwingiene ili kuonyesha heshima kwa uongozi uliopo katika ngazi jamii

Tafadhali alika na kuwasiliana pia na viongozi wa mitaa na wataalamu wa usawi wa jamii kwa ufafanuzi wa sera na sheria mpya ambazo ndugu na walezi wa SOS wanapaswa kufahamishwa endapo kuna mabadiliko yoyote.

2. Tukio la kujumuika pamoja na majirani wapya

Meneja wa mradi na mlezi wanapanga kikao kisicho rasmi katika nyumba/makao mapya na wazazi/walezi katika kitongoji. Meneja anafanya utangulizi mfupi wa kwa nini watoto wa SOS wanahitaji kurudi kwenye jamii yao, na anaomba ushirikiano wao. Mlezi anaelezea kazi yake na matarajio yake ya kujuana majirani zake wapya. Meneja anaondoka, na kikao rasmi zaidi kinaendelea, chai na chakula vinaweza kutumika. Mlezi anauliza jinsi anavyoweza kujifunza na kuheshimu majirani zake pamoja na mila na desturi za jamii mpya. Anauliza maswali yoyote kuhusu kuwa mama mlezi. Mwishoni mwa kikao, anawaalika majirani kwa sherehe ndogo baadaye, ambapo yeye na wazazi/walezi wengine hupanga shughuli na kucheza, ili watoto waweze kufahamiana. 

 

3. Kuwatambulisha watoto kwenye shule yao mpya

Mlezi wa mtoto/watoto wa SOS na mwalimu wa shule wanaweza kupanga kikao na mwalimu wa shule mpya ya mtoto. Baada ya utangulizi, mwalimu anaelezea mtazamo wa mtoto, uwezo wa kujifunza, na tabia yake awapo darasani. Mlezi anaelezea uwezo wa mtoto kihisia, kijamii na rasilimali zilizopo.

 Kwa wenye mahitaji maalum au wenye ulemavu, kama vile ulemavu wa viungo, tafadhali angalia mwongozo wa kuunganishwa, uk. 22.

 Siku ya kwanza ya kufika shuleni, mwalimu anamkaribisha mtoto na kuwaelekeza wanafunzi wenzake kumjumuisha kama rafiki. Kama mtoto anakubali, mwalimu anaweza kuelezea jinsi mtoto alivyoishi katika makao ya awali, na sasa anatarajia kupata marafiki wapya.

Kama makao hayapo mbali na shule, watoto wanaweza kuyatembelea, kujifunza kuhusu maisha katika makao, kucheza na kufanya shughuli za kijamii zilizopangwa.

Mpango Kazi C: Majadiliano ya kikundi na Mafunzo mahalia ili kupunguza adhari

  1. Tunawezaje kuunganisha mapendekezo haya ya awali katika hali yetu ya kila siku?
  2. Ili kuona na kuzuia adhari zinazoweza kutokea, tafadhali soma na ujadili utafiti wa Kisa Mafunzo Hiki cha mama mlezi wa SOS na binti yake.
  3. Tafadhali andaa mpango kazi wako kwa ajili ya kuingizwa kwenye familia ya malezi katika jamii.
  4. Tafadhali andaa mpango kazi wako wa mahojiano ya mara kwa mara kwa Wazazi na watoto baada ya kutoka.