Somo la 20/21

Ukurasa wa 7/7: Stadi nyingine muhimu kwa watoto na vijana balehe

Stadi nyingine muhimu kwa watoto na vijana balehe

Shughuli endelevu za kimazingira ya kiasili

Mkakati wa kijiji cha SOS 2030 unajumuisha wajibu wa kufundisha watoto katika shughuli za maisha. Katika kukua kwa viwanda na kukua kwa miji, maeneo mengi yanaharibiwa, na kuharibu uwiano baina ya watu na asili. Lazima kizazi kijacho kijenge ufahamu kuhusu kulinda mazingira ili kurudisha uwiano uliopotea. Mada hii inatoa visa-mikasa na shughuli za watoto ikiwa ni kwa jinsi gani wanaweza kujiingizia kipato kidogo kwa kuchakata taka za jamii ya vioo na plastiki kuweza kutengenezwa upya.

Katika mada nyingine, unaweza kupanga shughuli za kujifunza stadi za vitendo za bustani, kuelewa viumbe hai na kulinda mali asili kama maji, wanyama na mimea.

Teaching children and young people about their rights

Watoto katika malezi wana haki ya kuambiwa mambo yoyote yanayowahusu maisha yao, kama vile hatua za kutoka katika makao. Kwa mujibu wa Mkataba wa Haki za Watoto; watoto wana haki ya ”kujieleza kwa uhuru,  kuulizwa maoni yao juu ya mawazo yao, maisha na uwezo wao na kupata taarifa zao za msingi. Juhudi zifanyike ili kuwezesha kupata maoni yao na kupata taarifa kwa lugha pendwa na muafaka kwa watoto” Tazama ukurasa wa sita. Watoto wa afrika pia wanalindwa na Mkataba wa Watoto wa Afrika. Dr. Elvis Fokala anaelezea jinsi ya utekelezaji wa mikataba miwili ya watoto katika kaya, na majukumu jinsi walezi na wazazi waliyonayo kufundisha haki hizi kwa watoto wao.

Shughuli za kufanya watoto waelewe na kutekeleza haki zao katika malezi

Katika shughuli zao za kila siku, watoto siyo tu wafundishwe haki zao bali wajue jinsi ya kuziweka kwa vitendo katika familia zao. Hili linawezekanaje?

Huu ni mfano wa toleo la haki za watoto ambazo unaweza kuziandika na kubandika ukutani.

Kwa kuchukua haki moja baada ya nyingine  kisha kuijadili na mtoto kwa muda muafaka kunaweza kumfanya mtoto aielewe haki hiyo na maana yake. Kwa mfano unaweza kuwasilisha haki ya watoto kusikilizwa kuhusu maoni yao. Hii ina maanisha kuwa ni lazima washiriki na kujifunza kukubali maamuzi ya kila siku katika familia.

Shughuli za kuwafanya watoto wawe na sauti nyumbani

Kwa mfano, waulize watoto kila mmoja angependa aandae nini kwa chakula cha usiku,  na kwa nini anadhani ni muhimu kwa afya ya familia. Wakumbushe wasiingiliane wakati wa mazungumzo, ili wasikilizane kila mmoja. Kisha pigeni kura kwa uamuzi. Waambie kuwa wanaweza. Kwa mfano, waulize watoto kila mmoja angependa aandae nini kwa chakula cha usiku,  na kwa nini anadhani ni muhimu kwa aya ya familia. Wakumbushe wasiingiliane wakati ambapo kila mmoja anaongea, ili wasikilizane kila mmoja. Kisha pigeni kura kwa uamuzi. Waambie kuwa wanaweza.

 

 

Mpango Kazi Somo D: Majadiliano ya kikundi kupangilia shughuli

Kuna mambo mengi unapoanzisha maisha katika jamii, hivyo tafadhali jadili na kupangilia kwa umuhimu: ni mpangilio upi wa shughuli ungependa kuanza nao? Kisha panga mpango unaozingatia mahitaji yako.

Huu in muhtasari ambao unaweza kuuchagua:

  • Kufundisha stadi za kazi nyumbani na michezo kwa watoto au vijana balehe
  • Shughuli za kimaisha na bustani
  • Kufundisha watoto na vijana balehe kuhusu haki zao na jinsi ya kufanya kwa vitendo

Utakapochagua mada, tafadhali weka mpango unaoonesha ni kwa jinsi gani na muda gani utaitekeleza mada