Somo la 21/21

Ukurasa wa 3/6: Mada B: Kwa jinsi gani wamama wa SOS wameweza wamejandaa kwa kipindi cha mpito?

Mada B: Kwa jinsi gani wamama wa SOS  wameweza  wamejandaa kwa kipindi cha mpito?

Katika mada B utafanyia kazi mchakato muhimu wa kihisia wa maandalizi ya kuunganisha familia.Ni kwa jinsi gani wamama wa SOS watahisi wako salama na na  wana mwitikio chanya wakati anamkabidhi mtoto?

Ni kwa jinsi gani walezi wa SOS watajiandaa wenyewe kukabidhi mtoto?

Ni muhumu sana kwa walezi wa watoto wa SOS kuhisi wako salama na kushawishika kwamba kuunganishwa tena ni kwa maslahi mapana ya mtoto. Kwa mlezi aliyepata mafunzo hawezi kujifanya kuwa mtulivu wakati anamtoa mtoto kwa watu wengine isipokuwa mashaka na wasiwasi wote umejadiliwa na kutatuliwa kwa kina.

Kwa mlezi yeyote wa SOS mwitikio wake wa kwanza wa msingi katika kumrudisha mtoto kwenye familia yake inaweza ikawani moja ya huzuni, maumivu ya hisia kutokana na kutenganishwa na mtoto au kijana wake mpendwa. Pia hofu ya kwa jinsi gani kijana au mtoto ataonyesha mwitikio katika upya- Atapoteza hisia ya kuwa na uhusiano salama?

Hata hivyo kumuunganisha tena sio kusababisha maumivu ya kutenganishwa. Kukubali kwa dhati ni mchakato wa muda mrefu wa hatua kwa hatua wa kumshirikisha mtoto na ndugu zake, na kumsaidia mtoto kuongeza mahusiano mapya ambayo ni  salama  katika familia yake ya asili.Itachukua muda kuhama kihisia kutoka”Huyu ni mtoto wangu “na kuwa “Huyu ni mtoto wetu”.

 

 

Sikiliza mfano huu wa mafanikio katika shirikisho baina ya walezi wa SOS na familia,muda fulani baada ya familia kuungana tena, msichana mdogo alipewa ofa ya kurudi kwa mama yake wa SOS-kwenye kijiji cha SOS kwa muda wa mwezi mmoja –lakini alikuwa amejenga uhusiano wa karibu na mdogo wake wa kike ndio maana aliamua kurudi kwenye kijiji kwa muda.

Majadiliano ya vikundi dk 60

Tafadhali jisikie huru kushirikisha hisia zako, mashaka na matumaini yako:

  • Nini hisia zako binafsi ni zipi wakati unamtoa mtoto wetu kwa ndugu?
  • Nimeshawahi kupitia utengano mgumu katika maisha yangu ambao ukanifanya iwe ngumu kukubali?
  • Ninahitaji ushauri wa kisaikolojia ili niweze kukubali  watoto kuunganishwa tena?
  • Kwa jinsi gani kuungana tena kwa familia kutaathiri uhusiano wetu wa karibu na mahusiano na watoto?
  •  Kwa jinsi gani kuungana  tena kwa famila kutaathiri kazi yangu ya baadaye

Mada hizi zinaweza kujadiliwa mara kadhaa njiani mpaka makubaliano chanya yapatikane

Swali la msingi linalofuata: ni mambo gani ya kuzingatia wakati unamchagua mtoto au kijana kwaajili ya kuunganishwa tena?