Somo la 21/21

Ukurasa wa 5/6: Mada D: Ushirikiano wa wafanyakazi wa serikali, jamii na familia

Mada D: Ushirikiano wa wafanyakazi wa serikali, jamii na familia

Kushirikiana na wafanyakazi wa serikali za mitaa

Kurejesha katika nafasi nyingine kunahitaji ushirikiano wa karibu na wafanyakazi wa serikali ya mtaa na usimamizi wako kuhusu mtoto au kijana husika. Maamuzi yote ya kisheria kuhusu utambulisho rasmi wa mtoto lazima yapangwe na kutekelezwa Pamoja nao. Taratibu za kisheria na changamoto zake hutofautiana kutoka nchi moja hadi nyingine licha ya muda na mahitaji. Lengo ni kufanya muda wa kusubiri kuwa mfupi iwezekanavyo, pia ikiwa mtoto amewekwa katika familia ya muda kabla ya kuunganishwa tena.

 

 

 

Msimamizi wa eneo la SOSCV Hawassa, Ethiopia anaelezea jinsi wadau (wafanyakazi) wanavyoshirikiana na serikali za mitaa

Kuanzisha ujumuishaji mpya katika jamii

Kutayarisha viongozi wa jumuiya za kidini ni kazi nyingine muhimu. Kuelezea wazo la jumla la kuunganishwa ten ana kuimarisha huduma za mitaa itahakikisha mtazamo mzuri kwa mtoto na jamaa zake. Inaweza kutokea pia katika hafla za umma za karibu na kwa TV au redio.

 

Msimamizi wa eneo la SOSCV Hawassa, Ethiopia anaelezea jinsi tunavyowafahamisha viongozi wa jamii.

Kumuanzisha mtoto katika shule na elimu

Ili kuhakikisha kuunganishwa tena katika elimu, katika siku zijazo walimu wa shule ya msingi au wa shule za sekondari wanaweza kufahamishwa kuhusu mtazamo wa mtoto au kijana na stadi za jamii. Zingatia zaidi maelezo kuhusu ulemavu wowote wa kimwili au kujifunza na mahitaji maalumu.

Kulingana na hali hiyo, unaweza kumwomba mwalimu kumtambulisha mwanafunzi mpya, kabla na kuwahimiza darasa kumjumuisha kwenye mtandao wao. Hii inajumuisha kushughulikia aina yoyote ya chuki rika ambayo inaweza kutarajiwa. Ingawa uwazi kuhusu usuli ni mzuri, njia bora ya utangulizi ni kuheshimu matakwa ya mtoto au kijana.

 

Kuwezesha kurudi kwa familia ya asili

Ili kuanza kuunganishwa tena, ziara za ndugu kwenye kijiji zinaweza kupangwa.  Wakati wa ziara unaweza kupana shughuli za vitendo kama vile kupika chakula pamoja. Hii itakuruhusu kuona mwingiliano kati ya mtoto na wanafamilia na kuongeza kwenye uchunguzi wako kutoka kwa ramani ya mahusiano ya mtoto na vijana. Mtoto huwasiliana kwa njia ya uaminifu kuelekea kwa nani? Je, anamgeukia nani kwa msaada, usaidizi na ulinzi. Na, kwa nani inaonekana kuhisi kutokuwa salama, kuogopa, au kuepuka? Ukosefu wowote wa usalama unaweza kujadiliwa kwa uwazi na kutatuliwa.

Utaratibu huu utamtayarisha mtoto kwa muda wa kukaa katika familia.

    Majadiliano ya kikundi na mpango wa kazi

    Tafadhali jadili na upange

    • Je, tunawezaje kushirikiana na wafanyakazi wa serikali kutatua masuala yote ya kisheria?
    • Je, tunawezaje kujenga ufahamu wa kuunganishwa tena na viongozi katika jamii?
    • Tunawezaje kuwatayarisha walimu na marika kwa ajili ya kumkaribisha mtoto?
    • Tunaweza kuona jinsi gani mwingiliano salama na usio salama wakati wa ziara za familia?