Somo la 21/21
Ukurasa wa 4/6: Mada C: Kuchangua/kugundua mahusiano na uhusiano wa karibu wa mtoto au kijanaMadaC: Kuchangua/kugundua mahusiano na uhusiano wa karibu wa mtoto au kijana
Kitu gani kinatakiwa kijadiliwe na kupangwawakati wa kumchagua mtoto au kijana wa kumuunganisha na familia?
Na kwa jinsi gani tunaweza kufanya tathmini sahihi ya mahusiano ya kijamii ya watu?
Ni lini mtoto au kijana anakuwa tayari kuunganishawa na familia?
Kazi ya kuchagua mtoto au kijana wa kumuunganisha ni mchakato wa mtu binafsi. Kila kesi ni ya pekee. Kwaajili ya nyenzo za kufundishia (nadharia na vitendo) tumia muongozo huu.
Tafiti zinaonyesha kuwa moja ya kigezo muhimu sana katika kufanikisha zoezi la kuwaunganisha tena vijana na familia zao ni kuwa na mtandao wa uhakika wa kimahusiano
Kufanya maamuzi sahihi kuhusa kijana au mtoto inategemea maamuzi ya meneja na walezi wa SOS, ufahamu wao wa karibu nawa nndani kuhusu mtoto na ukaribu wa timu ya wafanyakazi. Kukusaidia kufanya maamuzi sahihi hapa kuna uzoefu fulani kutoka kwenye miradi ya kuwaunganisha tena na tafiti za kubadilisha wazazi. Hili ni jambo la jumla na linaweza lisifanye kazi kwa mtoto mmoja mmoja-tafadhali jumuisha maamuzi yako ya kitaaluma katika kila kesi.
Wakati gani mtoto au kijana anakuwa tayari kuhamishwa kwa walez?
Kwa ujumla watoto wa umri wowote wanastahili kuunganishwa na familia zao.Kiutendaji vijana ndio wanaunganishwa tena mara kwa maramara.
Mtoto anapokuwa mdogo inakuwa ni rahisi kuhama hutoka kwa mlezi mmoja kwenda kwa mwingine.Tafiti zinazonyesha kwamba watoto wadogo chini ya miaka mitatu mara nyingi wana uwezo wa kutengeneza uhusiano wa karibu ulio salama na walezi wapya. Baada ya Mwaka mtoto huyu atamtambua mlezi mpya kama mzazi wake wa kihisia na kumhamisha kutakuwa na mafanikio
Kwa watoto wa miaka mitatu mpaka miaka kumi na moja kuhama unaweza kuwa changamoto hususani kama alikuwa na muda mfupi wa kufungamanishwa na walezi wake wa SOS . Katika umri huu uimara wa kihisia na kimwili unahitajika kwaajili ya ujuzi,michezo na mafunzo endelevu . Tukio la kuhama laweza kusumbua uwezo wa kimasomo wa mtoto shuleni, na kuendeleza muunganiko wa kijamii pamoja na makundi aliyokuwa nayo. Mwishoni kuwaunganisha tena utahitaji kiwango cha juu cha hamasa kutoka kwa mtoto na kumpatia mtoto ujuzi katika familia
Vijana mara nyingi wana uwezo wa kuelewa na kuonesha nahitaji na natamanio yao na kufanya uamuzi wakiwa na ufahamu wa kutosha kuhusu familia zao kuunganishwa tena. Katika umri huu, ni jambo la asili pia kijitenga na malezi ya wazazi na kuanza maisha ya kujitegemea.Vijana wano uzoefu wa maisha nje ya kijij na mara nyingi wanamatamanio ya kuwa sehemu ya jamii. Hali y a balehe inaweza sababisha kukosa utulivu wa kihisia na kimwili, hivyo kusubiri ili wakomae ni jambo la kutilia maanani.
Watoto wenye mahitaji maalum au ulemavu mwingine
Kuunganishwa upya kwa watoto wenye ulemavu wa kimwili na kiakili ni changamoto kubwa katika jamii nyingi. Inapendekezwa kwamba miungano ya kwanza ya familia iwe na Watoto au vijana ambao wanastawi na wanaotarajiwa kuwa na uwezo wa kukabiliana na mabadiliko. Wafanyakazi itajenga uzoefu zaidi kwa ujumuishaji mgumu zaidi wa walemavu. Mwongozo huu wenye uzoefu katika Afrika Mashariki na kusini unaweza kusaidia kupanga michakato.
Majadiliano ya Kikundi dakika 30
Tafadhali jadili na ufanye mpango kazi kulingana na mawazo yako.
- Je, tuna maoni gani kuhusu umri wa mtoto au kijana husika?
- Ipi faida au hatari katika umri ambazo tunapaswa kuzizingatia?
- Utayari wa mtoto kuunganishwa tena: Je tunawezaje kutumia maarifa haya?
Unaweza kutumia zana kwa tathmini sahihi ya vifungo na viambatisho vingi vya mtoto
Jinsi ya kutumia ramani ya mahusiano ya mtoto na kijana
Tunawezaje kupata muhtasari wa vifungo na mahusiano muhimu zaidi ya mtoto, na kuelewa maoni ya mtoto mwenyewe kuhusu ni nani anayehusishwa naye kabla, wakati na baada ya kuunganishwa kwa familia?
Ni muhimu kwa wasimamizi na walezi kufanya tathmini yao wenyewe kuhusu mtoto yupi anashikamana naye. Pia, kujua
Maoni ya mtoto mwenyewe: ni nani anayehisi yupo salama na akiunganishwa naye na yupi anahisi kutokuwa salama akiunganishwa naye? Pia, ndugu wanaelezeaje uhusiano wao na mtoto? Tumia ramani hii itakusaidia kupata majibu kupitia mazungumzo.
Kiambatisho cha ramani ya mahusiano ni rahisi kutumia. Lengo ni kuwapa muhtasari wa wazi wale wote wanaohusika: mtoto au kijana anahusishwa na nani? Ni nani anayefanya ajiskie salama au sio salama?
Ramani inakupa pembe tatu za kutathmini ubora wa mtandao wa kijamii wa mtoto au kijana.
Mtazamo wa kitaalamu, mtazamo wa mtoto na mtazamo wa ndugu.
Tafadhali fungua na chapisha kiambatisho cha ramani ya mtoto na kijana. Chapisha kadri inavyohitajika na usome mwongozo kabla ya kuutumia.
Tunapendekeza kutumia ramani kwa kufuata hatua zifuatazo:
-
Mlezi wa SOS na wasimamizi wa programu Je, ni mtazamo wetu wa kitaaluamu kuhusu viambatisho muhimu vya mtoto au kijana huyu?
-
Kwa maoni ya mtoto: Mtu anayemfahamu mtoto au kijana huhoji na kutoa msaada wa kujaza ramani. Je, anaelezaje uhusiano wake muhimu ulio salama au usio salama?
-
Katika ziara ya nyumbani na ndugu: Wawasilishe na uwasaidie kujaza ramani. Je, wanaona vipi viambatisho vyao wenyewe kwa mtoto. Je, wanafikiri mtoto anawaonaje?
Mitazamo itabadilika wakati wa kuunganishwa tena, kwa hiyo tafadhali tumia ramani kabla, wakati na baada ya kuunganishwa kwa familia. Baada ya kutumia ramani katika mojawapo ya hatua tatu, tafadhali jadili na upange:
Majadiliano ya kikundi na mpango kazi wa dakika 45
-
Hayo maoni matatu (wataalamu, mtoto na familia) yanakubaliana au yanatofautiana.
-
Je, tutafanyaje ili kuunda makubaliano kati ya pande zote zinazohusika?
-
Je, tunawezaje kuimarisha viambatisho salama, na kutatua mahusiano yasiyo salama?
Ikiwa tathmini zako zilikufanya uamue kuendelea, ni wakati wa kupanga hatua inayofuata.
Kufanya kazi na wafanyakazi wa serikali na kuandaa jamii na familia kupokea mazingira ya kumlinda mtoto