Somo la 20/21
Ukurasa wa 1/7: Kuunganishwa kwa wazazi na watoto wa SOS katika jamii zao za asili - mwongozo kwa Wasimamizi wa programu na SOSKuunganishwa kwa wazazi na watoto wa SOS katika jamii zao za asili – mwongozo kwa Wasimamizi wa programu na SOS
Kwa wasimamizi wa programu za kuunganisha upya, tafadhali soma hii.
Utangulizi wa mada
Kipindi hiki kinatoa mfumo wa hatua kwa hatua kwa vikundi vya Walezi wa SOS na msimamizi wao au Meneja wa mradi kuhusu jinsi ya kujiandaa kwa kuondoka Vijijini/kwenye makao na kuwa Walezi wa jamii katika jamii zao wanazotoka.
Mada nne za kipindi zinaelezea jinsi ya kujenga usalama wa kisaikolojia kwa Walezi na watoto wao kabla, wakati na baada ya kutoka Kijijini/kwenye makao, kuishi kama familia za kambo katika jamii:
Mada A: Je, Walezi wa SOS wanawezaje kujitayarisha kikamilifu kwa ajili ya kwenda kuwa Walezi wa jamii?
Mada B: Je, tunawafahamishaje watoto na kuwashirikisha katika mabadiliko?
Mada C: Je, tunawasaidiaje watoto na vijana kujenga mahusiano mapya salama na watu wazima na wenzao katika jamii?
Mada D: Jinsi ya kutoa mafunzo kwa watoto na vijana mafunzo stadi kwa vitendo baada ya kuwa kwenye jamii.
Uwezo/umahiri wa kuoneshw
- Ushiriki wazi na matarajio katika mabadiliko kutoka kwa Mlezi wa SOS hadi mlezi wa makao ya SOS.
- Kuunda kikundi kwa ajili ya kushiriki na kupanga pamoja – kabla, wakati na baada ya kuhama.
- Ujuzi wa kuwafanya watoto wajisikie salama katika awamu zote za mpito.
- Ujuzi wa kuhakikisha haki za watoto katika mchakato.
Lengo la mada
-
Mada hii itakusaidia kufanya kazi pamoja, na kuandaa mabadiliko ya kisaikolojia na uhusiano kutoka kwa maisha ya zamani hadi maisha mapya kama Mlezi wa makao ya SOS katika jamii yako.