Somo la 21/21
Ukurasa wa 1/6: Kuunganisha watoto na familia zao za asiliKuunganisha watoto na familia zao za asili
Tafadhali soma huu mwongozo wa meneja programu na walezi wa SOS
Utangulizi wa mada
Mada hii inatoa mwongozo wa hatua kwa hatua muendelezo wa vikao wa pande zote katika uunganishaji wa mtoto. Vikao hufanywa na meneja mmoja au zaidi wa programu ya uungamishaji wa watoto katika makao ya SOS CV pamoja na kina Walezi wa SOS. Masomo manne katika mada yanayoelezea hatua nne kwenye mpango wako ni:
Somo A: Utangulizi wa uunganishaji
Somo B: Jinsi gani kina Walezi na wafanyakazi wa SOS wanavyoandaa na kipindi cha mpito?
Somo C: Uandaaji wa uhusiano na kujenga ukaribu na mtoto
Somo D: Uhusiano wa watendaji wa serikali, jamii na familia
Somo E: Kupunguza hatari kwa kufanya ufuatiliaji baada ya kumuunganisha mtoto na familia yake
Ujuzi unaotakiwa
- Elimu ya kuungamanisha familia
- Ujuzi wa kuwafanya walezi, watoto na ndugu zao wajihisi salama katika mchakato
- Tathmini ya hali ya mtoto ya sasa na mahusiano baada ya kuungamanishwa
- Uhusiano wa serikali, jamii na ndugu
- Kupunguza uwezekano wa hatari wakati wa uungamanishaji
Lengo la mada
Mada hii itakusaidia kufanya kazi pamoja, na kuwandaa kisaikolojia na uhusiano bora kwenye kijiji, ili kufanya watoto waunganishwe vizuri na wazazi au ndugu zao.