Somo la 21/21

Ukurasa wa 2/6: Mada A – Utangulizi wa uunganishaji

Mada A – Utangulizi wa uunganishaji

Maana ya uunganishaji wa familia

Kwa Muongozi wa Azak zisizo za kiserikali ndiyo muongozo wa uunganishaji :

Mchakato wa kumuunganisha mtoto na familia yake (familia ya asili) aliyejitenga nayo unatarajiwa kuwa ni wa kudumu, ili apate ulinzi, uangalizi na kutambuliwa katika kila eneo la maisha”

Katika hii mada, tunalenga kuelewa na kuandaa uunganishaji wa mtoto na famillia, wazazi au ndugu. Njia nyingine za uunganishaji familia ni kama

  • Mtoto anaweza kupelekwa kwa mlezi wa SOS (Mada hii iko katika mada 20)
  • Mtoto anaweza kuondoka katika malezi mbadala na kwenda kujitegemea kwenye jamii (Hii imo katika somo la 14 na 15)
  • Mtoto anaweza kuasiliwa kisheria na famiilia. (Njia hii haitumiwi na vijiji vya SOS)

Kwanini kuwaunganisha tena watoto na vijana ni kipaombele?

Ni mkakati mpya wa SOSCV 2030 kuwaunganisha watoto na jamii, njia ya kumshirikisha mtoto ni muhimu sana. Kipaombele cha kwanza cha mkakati huu ni kuhakikisha  haki ya watoto katika kutambua utamaduni wake,familia na jamii yake kwa ujumla

Miaka ya nyuma watoto na vijana katika makao salama walikuwa wanalindwa kutoka kwenye hatari za jamii na kutelekezwa kwa watoto.  Mahusiano yao muhimu ya kihisia yalikuwa kwa walezi wao wa SOS na kwa watoto wengine ambao walikuwa wanaishi nao paamoja kwenye nyumba hizo. Asante kwa wazazi na walimu, matokeo yamekuwa ya ufanisi mkubwa.

Kwanini   kuunganishwa tena kunahitajika? Ingawaje muundo wa malezi ya kwenye makao uliboresha maendeleo ya mtoto katika kundi dogo la watoto, haukuimarisha uwezo wa jamii husika kulea watoto wote.Pia walezi wa SOS na watoto walitengwa na jamii.Kwa watoto wadogo walioondolewa na kuunganishwa na ndugu zao na maisha ya jamii ilikuwa ni changamoto baada ya kukua katika eneo salama.

Mkurugenzi wa vijiji nchini Ethiopia,Sahlemariam Abebe, anaeleza kipaombele kipya:”Idadi ya watoto walio katika hatari inaongezeka kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa na matatizo mengine ambayo yanatokana na msongo wa mawazo .  Badala ya kutumia gharama kubwa katika suluhisho la watoto wachache waliotengwa, lazima kuijengea jamii uwezo kwa ujumla hata kama itatubidi kupunguza viwango vya matunzo kwa kila mtoto. Kufanya hivi kunahitaji mabadiliko magumu ya kifikra na kimtizamokwa wote: “Leo  hii wazazi ambao wapo katika hatari kwenye jamii wanafikiri  kwamba kijiji ni suluhisho zuri kwa watoto wao.Wamama wa SOS wanaogopa kwenda nje , na kukabiliana na tamaduni za eneo husika na lugha.Watoto na vijana wana uhusiano wa kina na mama zao hivyo wanaogopa kutenganishwa na walezi wao   na kuanza kuishi na familia zao za asili.

 

Mjadala kwenye kikundi dk 15

  • Tunawaza nini tunaposikia kuunganishwa tena?
  • Faida zipi na changamoto zipi ambazo tunaweza tukaziona wakati wa mchakato?
  • Tafadhali kubali mambo matatu ni wapi utahitaji msaada kutoka kwenye uongozi.

    Ni ipi nafasi ya mtoto katika kumuunganisha tena na familia?

    Kumpa nafasi mtoto maana yake ni sauti za watoto na vijana walio katika malezi kusikilizwa katika hatua zote wakati wa maandalizi ya kuishi na ndugu.Wanatakiwa kuwa washiriki halisi na wenye ushawishi wa kweli katika kupanga na kutoa maamuzi. Lazima wawe na usemi katika kuhamisha hisia zao na ukaribu kwa walezi wao wa SOS na rafiki  zao ndani ya kijiji, kuunda uhusiano salama mpya na ndugu zao na majirani.Wakati wakiwa kwenye malezi lazima jitihada zifanyike kufuatilia na kuwaunganisha watoto na ndugu zao.

     

     

     

    Katika umri wa miaka 34,mtoto aliyekuwa anaishi kwenye kijiji Eschalew sasa hivi amefanikiwa kuwa mfanyabiashara.Bado anakumbuka maumivu ya mambo aliyokuwa anafanyiwa kwenye kijiji alichokuwa analelewa ambapo ndugu hawakuruhusiwa kwenda kumtembelea, baadaye familia yake iliruhusiwa kumuona lisaa limoja kwa mwezi.Tigist-ambaye sasa ana miaka 25-alikuwa mdogo na alifurahi kuwaona ndugu zake muda wote wakati alikuwa anaishi kwenye kijiji.

    Kanuni nne za kutuongoza kufanikisha familia kuungana tena

    Katika  tafiti za Africa na kimataifa, zimeeleza kwa ufupi mambo muhimu ya mahusiano na uhusiano wa karibu  kwa watoto na walezi wao. Kadiri mambo haya yanapofikiwa/kutimizwa pindi mtoto anapokuwa katika umri mdogo inaleta mafanilio makubwa kwa mtoto akiwa mtu mzima katika elimu,ujuzi wa kila siku na uwezo wa kuwa  na mtandao wa kijamii. Kanuni nne zinaweza kuongoza  kazi yetu katika kuhama kutoka maisha ya kijiji kwenda kuunganishwa na ndugu.Katika mchakato mtoto anahitaji:

    • Uhusiano wa karibu wa kihisia na mlezi kwa muda mrefu,na kumsaidia kwenda kwa wengine.
    • Kuwa mwanachama anayekubalika katika kundi jipya la vijana
    • Mtoto pamoja na walezi wake lazima wawe washiriki wazuri Lazima kuwe na makubaliano kati ya wenye uhusiano wa karibu na wale wanaofanya maamuzi juu ya maisha yao:Wasimamizi(managers),walezi wa SOS,wazazi na ndugu,walimu wa shule na wanajamii.

      Majadiliano ya kikundi dk 20

      • Tafadhali jadili: tunawezaje kutumia hii miongozo katika mipango yetu ya kuwaunganisha tena?