Somo la 13/19

Ukurasa wa 2/5 Mahitaji ya mtoto ya kukutana na wazazi halisi na makubaliano kati ya wazazi na familia mlezi

Mahitaji ya mtoto ya kukutana na wazazi halisi na makubaliano kati ya wazazi na familia mlezi

Watoto walio katika malezi wana familia mbili:familia yake ya asili na ile inayomlea. Utafiti kwenye huduma za malezi inaonyesha kwamba kuna malengo mawili muhimu ambayo unapaswa kuyatimiza:

  • Watoto wanaolelewa mbali na familia zao huwa hawafanyi vizuri katika maisha kama watapoteza mawasiliano yote na familia yao halisi wakati wanaishi katika familia mlezi. Mwishoni mwa malezi, watoto waliolelewa mara nyingi hawana wa kumgeukia ila familia halisi. Kama hawakuwa na mawasiliano na wazazi wao wakati wakiishi katika familia mlezi, wanaweza pia wakapoteza uhusiano huu.
  • Jinsi ambavyo utajenga makubaliano na heshima zaidi kati ya familia mlezi na wazazi halisi, ndivyo mtoto atakavyojisikia salama zaidi: kucheza, kuchunguza na kujifunza. Kama una mgogoro na wazazi halisi – au kuonyesha kutowaheshimu –nguvu ya mtoto itatumika kujisikia kutokuwa salama na ataumia kutokana na kutokuwa na msingi salama.

 

Hii ni mojawapo ya kazi ngumu kwa wazazi walezi: kumchangia mtoto na wengine ambao hawawezi kumtunza mtoto wao. Kwanini kazi hii ni ngumu sana? Hebu tuangalie ni kwanini watoto wanapawekwa mahali pa kulelewa, na nini hasa hali ya wazazi wao halisi, na kisha tuangalie mbinu za kuwezesha mawasiliano na wazazi.